The House of Favourite Newspapers

Mastaa Hawa Wametoka Relini

Weusi

KUTOKA relini ni moja kati ya misemo inayotumiwa sana na watoto wa ‘dijitali’ ikiwa na maana kuwa juu na ghafla kupotea. Kutoka relini huku inawezekana ulikuwa na pesa na baada ya kipindi ukawa huna kitu au unaweza kutamba kwa muda f’lani kwenye gemu na baada ya kipindi ukawa husikiki kama ilivyokuwa awali.

Katika muziki wa Bongo Fleva nao kuna wasanii ambao wametoka relini. Walikuwa wakitamba na kukubalika kila wakitoa nyimbo zao lakini kwa sasa Tangu mwaka uanze, ameshatoa ngoma kibao zikiwemo Amsha Popo, Kaa Mbali Nao na Mikono Juu lakini bado zimemtoa nje ya reli.

Weusi

Huwezi kutaja makundi ya Muziki wa Hip Hop Bongo ukaacha kulitaja Kundi la Weusi kutoka Arusha likiwa na vichwa ‘hatari’ kama vile Nikki wa Pili, Joh Makini pamoja na G Nako. Ngoma zilizow-aweka relini ni Gere, Nusu Nusu na Nje ya Box.Wakali hawa kwa muda mrefu wameweza kuteka Muziki wa Hip Hop Bongo na kufanya shoo kibao za ndani ya nchi.

Walianza kutoka relini taratibu baada ya kuachia Ngoma ya Madaraka ya Kulevya ambayo haikupokelewa kama zilivyokuwa ngoma zao za zamani, wakaachia Ni Come ambayo kideo chake kiliwakusanya mastaa kibao kama vile Vee Money, Jux, Nandy, Idris Sultan lakini napo ikaonekana ya kawaida.

Kwa sasa wameachia ngoma nyingine iitwayo Mdundiko ambapo bado haijawaonesha kurudi relini kama zamani.

 

Shilole

Alipoingia rasmi kwenye Bongo Fleva akitokea Bongo Movie, wengi walimtabiria kufika mbali kutokana na ‘kujichetua’ kwake hasa inapotokea yupo jukwaani. Ngoma ya Say My Name aliomshirikisha Barnaba ndiyo iliyomuweka kwenye chati ikifuatiwa na Namchukua, Malele na Hatutoi Kiki.

Shilole ama Shishi Baby kama anavyopenda kujiita alikuwa relini kweli, ukiachilia Muziki wa Mduara aliokuwa akifanya, uhusiano wake na ‘viben’ten’ ulimfanya kuongelewa kila kona.

Tangu afunge ndoa na Ashraf Uchebe mwishoni mwa mwaka jana kumemfanya kutoka nje ya reli. Hajaonekana jukwaani akipafomu, kwenye redio na TV hasikiki kwa nyimbo wala uhusiano wake.

Ruby

Alipotoa Ngoma ya Na Yule akiwa mmoja kati ya zao la Jumba la Kukuza Vipaji ‘THT’ wengi walimtabiria kufika mbali hasa kutokana na uwezo wa kucheza na sauti yake. Ruby alikuwa Ruby kweli! Alikuja kufunika na ngoma nyingine ya Forever kisha Sijutii na Nivumilie alioshirikishwa na Barakah The Prince.

Alianza kutoka relini taratibu baada ya kujitoa THT, akaachia Ngoma ya Walewale ambayo haikuwa juu kama za awali. Kwa sasa anadaiwa kurudi tena THT ambapo ameshaachia Ngoma ya Niwaze akiwa amewashirikisha wakali wa R&B Bongo, The Mafik.

Malaika

Alianza kukaa relini alipoachia kwa mara ya kwanza ngoma yake ya Sare akimshirikisha Prodyuza Mesen Selekta.

Malaika ambaye alianza kuonekana kwa mara ya kwanza kupitia Ngoma ya Uswazi Take Away ya Chegge, uwezo wake wa kucheza na sauti ulimfanya kuwa relini hasa alipoachia ngoma yake ya pili ya Rarua.

Ngoma hizo mbili, Sare na Rarua zilimpelekea kufanya shoo kibao ndani na nje ya nchi hususan Marekani. Maisha yanakwenda kasi sana! Kwa muda mrefu sasa hajarudi relini kama zamani. Kitaa ameachia Ngoma ya Haachi lakini bado haijamfanya kurudi relini kama zamani.

Wengine

Listi ya wasanii wengine ambao walikuwa relini na sasa wametoka, hawasikiki kama zamani licha ya kuendelea kutoa ngoma ni Ben Pol, Pam D, Young Killer, Young D, Izzo B, Aslay na Mwasiti.

Stori: Andrew Carlos

Comments are closed.