Mastaa KMC Wapewa Program Maalumu Kuimaliza Yanga

UONGOZI wa KMC umeweka wazi kuwa kwa sasa mastaa wa timu hiyo ikiwa ni pamoja na Miraj Athuman, Awesu Awesu, Juma Kaseja wamepewa program maalumu kwa ajili ya mechi zao zijazo ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Yanga.

 

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kutokana na timu za taifa kuwa na mechi kwa ajili ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia na wachezaji waliobaki wamepewa program maalumu kuwa tayari kwa ajili ya mechi zijazo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala alisema kuwa tayari benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, John Simkoko na msaidizi wake Habib Kondo pamoja na Hamadi Ally wana program maalumu kwa wachezaji wao.

 

“Maandalizi yameanza ambapo kwa sasa makocha wetu wametoa program maalumu kwa wachezaji wetu kikubwa ni kuona kwamba tunashinda mechi zetu zijazo ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Yanga ambayo tutacheza Uwanja wa Majimaji, Songea.

 

“Hatujaanza vizuri msimu wa 2021/22 kwa kuwa mchezo wa kwanza tulipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Tanzania na mchezo wa pili tulilazimisha sare mbele ya Coastal Union hivyo tupo tayari kwa ajili ya ushindani,” alisema Mwagala

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam


Toa comment