The House of Favourite Newspapers

MASTAA KUOPOA NJE YA NCHI NI FURSA AU MAPENZI YA DHATI?

IMBI la mastaa wetu kuopoa wapenzi kutoka nje ya nchi limezidi kushika kasi. Kwa nyakati tofauti, staa wa Bongo Fleva, Ally Salehe Kiba ‘AliKiba’, Ambwene Yesaya ‘AY’, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na sasa tunamuona kijana Ben Pol, wanafanya hivyo.  

 

Kwa hivi karibuni, Ben Pol amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuanika penzi lake jipya na mwanadada kutoka Kenya aitwaye Anerlisa. Inaelezwa kuwa, mrembo huyo walikutana kwenye ‘event’ ambayo iliandaliwa na mrembo huyo nchini Kenya. Mara baada ya kukutana, kubadilishana namba, wawili hao walianza kuyajenga taratibu kabla ya kuamua kujilipua kwenye mitandao ya kijamii wakila bata nchini Kenya.

 

Mrembo huyo anatajwa kuwa anatoka familia bora huku mwenyewe akiwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya maji yaitwayo Executive Still Water. Kuonesha kwamba penzi lao lipo ‘fire’, msimu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, wawili hao walikwea pipa na kwenda kula bata Ufarasa na Dubai. Penzi hili limechipukia ghafla kama lilivyoibuka la Diamond ambaye aliaminika ana uhusiano na Kim Nana, fasta tu akabadili gia angani.

Ben Pol alikuwa na mwanamke mwingine ambaye alizaa naye lakini ghafla, akahamishia majeshi kwa mrembo wa Kenya. Swali la kujiuliza hapa, vijana hawa wamekwenda kuopoa nje ya nchi wakiwa na mapenzi ya dhati au kuna fursa fulani ambayo wameichungulia?

 

Mijadala mbalimbali mitandaoni imewataja kua baadhi yao ni kweli wamechukua wanawake kutoka nje kwa mapenzi ya dhati lakini wengine wametajwa kuwa ni fursa. Kwa waliotajwa kuwa wamechukua kwa mapenzi ya dhati ni wale ambao wanaonekana kufikia hatua ya kuoa ambapo katika orodha hiyo wapo AY, AliKiba na AY wametajwa kuwa wana mapenzi ya dhati kwa kwa kigezo kwamba wameoa huku Diamond na Ben Pol wakidaiwa eti hawana mapenzi ya dhati bali ni fursa.

 

DIAMOND

Kabla ya kuanza uhusiano na Tanasha, mrembo kutoka Kenya, alikuwa na mrembo wa Kiganda Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye alimuahidi kumuoa lakini hakufanikisha suala hilo. Diamond na Zari walidumu kwenye uhusiano kwa miaka kadhaa na kufanikiwa kuzaa naye watoto wawili.

 

Kama hiyo haitoshi, Diamond huyohuyo aliwahi kumuahidi kumuoa Wema, akatangaza mbwembwe kama zote lakini mwisho wa siku akamuacha solemba. Historia hiyo ya kuahidi na kutotekeleza inampunguzia maksi za kuaminika Diamond kwani ana orodha ya warembo wengi ambao amewapitia bila kuonesha msimamo wa ndoa.

 

BEN POL

Vivyo hivyo kwa Ben Pol, licha ya kuwa msiri sana kwenye suala la uhusiano, kitendo cha kummwaga ghafla mzazi mwenzake na kuonekana na kifaa kutoka Kenya, kinampunguzia maksi za kuaminika. Imeelezwa pia, Ben Pol ameitumia fursa ya kuwa na mrembo huyo kama eneo la kujitangaza kimuziki nchini Kenya ambapo tayari wameshafanya shoo kadhaa nchini humo.

 

NI FURSA?

Wachambuzi wa mambo ya burudani mara kadhaa wamekuwa wakisema Diamond amekuwa akiwatumia warembo hususan wa nje ya nchi kwa kigezo cha kuongeza wigo wa kibiashara. Wanaeleza kuwa, alifanya hivyo kwa Zari ambaye alikuwa na mtaji wa watu Afrika Kusini, vilevile nyumbani kwa mrembo huyo Uganda. Hivyo kitendo cha yeye kutembea na Zari, atazungumzwa na vyombo vya habari vya Afrika Kusini pamoja na Uganda.

 

TUJIFIKIRISHE ZAIDI

Mwishoni mwa mwaka jana, Diamond alitangaza kumuoa Tanasha Februari 14, mwaka huu na watu kusubiri kwa hamu lakini hata hivyo juzikati jamaa ametangaza kuahirisha ndoa hiyo hadi pale atakapoitangaza tena jambo ambalo linazidi kutia shaka kama kweli jamaa ataoa au la.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO


Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.