Mastaa: Magufuli ametuua kwa njaa

Kabula (1)GLADNESS MALLYA

Jambo limezua jambo! Kufuatia tumbuatumbua inayoendeshwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa vigogo waliokuwa wanawapa jeuri mastaa wa kike mjini, wenyewe wameibuka na kusema kiongozi huyo ‘amewaua’ kwa njaa.

Chanzo makini kililiambia gazeti hili kuwa mastaa wengi wa kike wanalalamika njaa na ndiyo maana tangu alipoingia madarakani Rais Magufuli na kuanza kuwaondoa mafisadi, wasanii hao wamekuwa hawaonekani viwanja kama zamani kwa sababu hawana mkwanja.

“Yaani wasanii wa kike wana hali mbaya sana ndiyo maana hamuoni wakiwa na mbwembwe kama zamani wamekuwa wakijifungia ndani tu hawataki kuonana na watu kwani hata hela za kwenda saluni kujiremba hamna maana wanasema waliokuwa wakiwapa jeuri wengi wao wamekumbwa na tumbua majipu,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kupata ubuyu huo, paparazi wetu aliwatafuta baadhi ya mastaa ambapo walikuwa na haya ya kusema;

ISABELA.pngISABELA MPANDA

“Kweli tumeathirika sana na hii tumbua majipu maana waliokuwa wakitupa fedha nyingi hata ukiomba milioni wanatoa kwa sasa wanaogopa hata ukiwapigia simu hawapokei huku wengine wakiwa ni wale vigogo waliokamatwa, Rais Magufuli ametunyoosha.”

madahaBABY MADAHA

“Kiukweli lazima iathiri kwa sababu ilikuwa rahisi kwa mtu kudhamini hata katika muvi. Kipindi cha Kikwete (Jakaya, Rais wa awamu ya nne) mtu anakupa milioni 20 au 30 kwenye muvi lakini sasa hivi, thubutu.”

jini_kabula
MIRIAMU JOLWA ‘JINI KABULA’

“Mimi sina kawaida ya kutoka na mapedeshee, bwana’ngu ni wa kawaida sana kwa hiyo sijui kama imeathiri vipi hiyo tumbua majipu.”


Loading...

Toa comment