The House of Favourite Newspapers

MASTAA MMEMSIKIA MZEE WA UPAKO?

 

KATIKA moja ya mafundisho yake kanisani kwake, Ubungo-Kibangu jijini Dar, siku chache kabla ya kuingia Mwaka Mpya wa 2019, mchungaji Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ alitumia dakika zaidi ya kumi kueleza kile alichokiita ni ‘ujinga’ wa mastaa wa tasnia mbili za Bongo Muvi na Bongo Fleva.

 

ALISEMA NINI?

Mzee wa Upako, akionekana kuchukizwa na jambo, alidai kwamba, siku chache kabla ya

mafundisho yake hayo alikutana na vijana aliodai kuwa wanajiita masupastaa wa Bongo Muvi na Bongo Fleva.

 

Katika mambo yaliyomshangaza ni kwamba ili kuwa supastaa lazima usuke nywele, uvae hereni na kuvaa suruali chini ya makalio kwa mtoto wa kiume!

MSIKIE MZEE WA UPAKO

Alisema baada ya kuwaona mastaa hao alikumbuka: “Mimi miaka ya 1970 wakati ninakua, mwanaume au kijana wa kiume ukisuka nywele, mama yako atatafuta mtaa wa kwenda kuishi.

 

Atafukuzwa mtaani kama mbwa koko (mbwa anayerandaranda ovyo), siyo kijana mwenyewe, lakini yeye na mama yake watafukuzwa kama mbwa koko.“Kule kwetu Iringa tulikuwa na watu walioitwa Wahindi koko na mbwa koko.

 

“Ilikuwa kijana wa kiume ukivaa hereni, hata shule unayosoma ilikuwa unafukuzwa kama mbwa  koko.“Leo, eti ili uonekane wewe ni supastaa ni lazima uvae hereni na kusuka nywele na Basata (Baraza la Sanaa la Taifa) ipo na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ipo. Huo ni ujinga kwani hawa vijana wanakua.“Mimi huwa ninajiuliza,KIJANA ambaye leo anavaa hereni,  maumivu ambayo wake wanayapata kuwa na kijana wao wa kiume.

 

Inafika usiku dume zima unaanza kufumua nywele! Mke au dada yako anafumua nywele na wewe unafumua nywele!“Mke wako au dada yako anavua hereni na wewe kijana wa kiume unavua hereni! Huo utamaduni wa wapi kama siyo upuuzi?“Kijana ambaye leo anavaa hereni, maumivu ambayo wazazi wake wanayapata kuwa na kijana wao wa kiume anayevaa hereni, atayapata kijana huyo siku mtoto wake wa kiume atakapokuwa amevaa hereni kwani mtoto wa nyoka huzaa nyoka.

 

“Ningekuwa mimi nina uamuzi katika Serikali, kijana yeyote wa kiume, mwanamuziki au mwigizaji wa sanaa, fi lamu yake au wimbo wake nisingeupitisha kama huwa mhusikaanavaa hereni au anasuka nywele”.

 

ISHARA ZA USHOGA

“Kusuka nywele na kuvaa hereni ni ishara za ushoga, kuna roho wa ushoga anawatafuta watu wetu. Hiisiyo salama hata kidogo, kuna roho wa uovu anawaandama bila wenyewe kujua.”

 

MASTAA MMEMSIKIA MZEE WA UPAKO?

 

Katika hilo, kwa mujibu wa waliomsikiliza Mzee wa Upako, walimuunga mkono na kutamani ujumbe huo ungewafi kia mastaa wa Bongo Muvi na Bongo Fleva wanaosuka nywele na kuvaa hereni.

 

Walisema kuna mifano ya mastaa wengi wa Bongo Fleva waliofanya na wanaofanya vizuri ambao huwezi kuwaona wakiwa wamesuka nywele wala kuvaa hereni kama Profesa Jay, Sugu, King Kiba, AY, Roma na wengine wachache.

 

Yapo mambo mengi ambayo wasanii huigwa na jamii hasa vijana wanaoamini wasanii ndiyo  wanaokwenda na wakati.Ilielezwa kuwa, miongoni mwa mambo hayo yanayoigwa ni namna ya uvaaji, aina za nguo na staili fulani za nywele kama kusuka kunakofanywa na wasanii kama Jux, Diamond  Platnumz, Rayvanny, Harmonize na wengine.

 

Wengi wanaamini kuwa tatizo linalojitokeza kwa baadhi ya mastaa hao ni elimu ndogo na wengine ni ulimbukeni tu wa ustaa hivyo ni vema kila mmoja akajitathmini upya na kukumbuka kuwa nyuma yake  kuna jamii inayomuiga kile anacho kifanya.

Comments are closed.