The House of Favourite Newspapers

Mastaa Simba Waahidi Ushindi Leo Dhidi ya Vipers Ugenini

0
Wachezaji wa Simba wakiwa kwenye mazoezi ya mwisho katika uwanja St. Mary’s tayari kuivaa Vipers ya Uganda mchezo wa kundi C ligi ya Mabingwa Afrika.

 

MASTAA wa Simba wamesema kuwa safari hii hawaachi kitu Uganda mara baada ya kushindwa kupata matokeo katika michezo michezo miwili mfululizo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Simba leo Jumamosi wanatarajiwa kukipiga dhidi ya Vipers ukiwa ni mchezo wa tatu kwao kuucheza kwenye mashindano hayo ambayo wamepangwa Kundi C, huku wakiwa wametoka kupoteza katika michezo miwili mfululizo dhidi ya Horoya na Raja Casablanca.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mshambuliaji wa timu hiyo, Moses Phiri alisema: “Tunaenda Uganda kwa ajili ya kuhakikisha kuwa tunapata matokeo mazuri kutokana na kushindwa kupata matokeo mazuri katika michezo yetu iliyopita, najua tunakwenda kukutana na upinzani mkubwa kwa Vipers lakini lazima tupate matokeo.

 

“Kwa sasa najua mashabiki wetu wanavyoumia na matokeo lakini kwa sisi kama wachezaji tunawaomba wavumilie kwani furaha itarejea na kupitia mchezo huu tutawafurahisha.

 

” Naye kiungo mshambuliaji, Mzambia Clatous Chama alisema: “Tuna kila sababu ya kupambana kwa ajili ya timu, hatutaki kusema kuwa kwa kuwa tupo ugenini basi tusubiri mechi za nyumbani, hapana tunahitaji kila pointi katika kila mchezo wetu wa mbeleni, hivyo tutapambana kuhakikisha kuwa tunapata matokeo mazuri Uganda.”

STORI: MARCO MZUMBE

Leave A Reply