The House of Favourite Newspapers

Mastaa Simba Wapigishwa Tizi Kwenye Jua Kali

0

PABLO Franco, Kocha Mkuu wa Simba  Ijumaa aliwafanyisha mazoezi wachezaji wake kwenye mchana wa jua kali ikiwa ni maandalizi ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) dhidi ya Dar City unaotarajiwa kuchezwa kesho Jumapili, Uwanja wa Mkapa.

 

Kocha huyo sambamba na msaidizi wake, Selemani Matola waliwafanyisha mazoezi hayo mida ya saa nane mchana mastaa hao ambapo mazoezi hayo yalifanyika Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju jijini Dar.

Miongoni mwa mastaa waliopo katika mazoezi hayo ni Chris Mugalu, Pascal Wawa, Gadiel Michael, Kenedy Juma, Yusuph Mhilu, Erasto Nyoni, Meddie Kagere, Hassan Dilunga, Aishi Manula, John Bocco na Pape Sakho.

 

Kwenye mazoezi hayo, Pablo alikuwa akiwasisitiza wachezaji wake hasa safu ya ushambuliaji kuwa makini katika kutumia nafasi ambazo wanazipata. Mabao aliyokuwa akisaka Pablo ilikuwa ni kupitia pembeni kwa Gadiel ambaye alikuwa na kazi ya kupiga krosi kati.

Bernard Morrison, Mohamed Hussein, Henock Inonga, Jonas Mkude na Rally Bwalya hawakuwa sehemu ya wachezaji waliohudhuria mazoezi hayo.

 

Katika hatua nyingine mastraika wawili wa Simba, John Bocco na Chris Mugalu jana walitoa gundu la kutofunga kwa siku 193.

Wawili hao walifunga mabao kwenye mazoezi ya timu hiyo ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Dar City kwenye Uwanja wa Simba Mo Arena, Bunju.

Bocco alifunga bao moja kwa kichwa akitumia krosi iliyopigwa na Pape Sakho na Mugalu pia alifunga bao kwa pasi ya Pape kwa kichwa ndani ya 18.

Pia Mugalu alifunga bao akiwa kwenye mwendo baada ya kukokota mpira akiwa nje ya 18 na kufunga kwa shuti lililomshinda kipa Aishi Manula.

Waandishi Wetu, Dar es Salaam

Leave A Reply