The House of Favourite Newspapers

Mastaa Sita tu Wakomba Dakika 180 Yanga

0

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kwa asilimia kubwa anafurahia uwezo wa wachezaji wake na anaamini kwamba atatengeneza kikosi imara kitakachokuja kuwa tishio kwa Afrika, baada ya mastaa sita tu kumalizika dakika 180 kwenye mechi mbili.

 

Tayari mpaka sasa Nabi amewaongoza vijana wake kwenye mechi mbili za ligi na zote wameweza kusepa na pointi tatu na kumfanya afikishe pointi sita na mabao mawili ambayo yanaifanya Yanga kuwa nafasi ya pili kwenye msimamo kinara ni Polisi Tanzania yenye mabao manne.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Nabi alisema kuwa anawatambua wachezaji wake kuhusu uwezo wake na tayari yupo kwenye mpango wa kusuka kikosi imara kitachofanya vizuri kwenye mashindano ya ndani na nje.

 

“Kiufundi nasema kwamba wachezaji ambao wapo Yanga wote ni imara na bora kwa sababu walisajiliwa na kamati ambayo ilikuwa inawajua wachezaji. Katika hilo ninajivunia kwani hata mimi nilikuwa kwenye hiyo kamati hivyo nina amini kwamba muda ukiwadia tutakuwa na kikosi imara sio hapa ndani bali Afrika.

 

“Ninachokifanya kwa sasa kwenye mechi zote ni kuweza kuwa na mzunguko ili kuwapa nafasi wachezaji wote wacheze na hicho ndicho ninachokitaka, nawaambia mashabiki watulie mimi ni mtu wa matokeo na sio manenomaneno,” alisema Nabi.

 

Tayari Nabi kuna wachezaji ambao wanaonekana kupenya jumla kikosi cha kwanza na kwenye mechi mbili za ligi mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba na ule dhidi ya Geita Gold, Uwanja wa Mkapa walianza kikosi cha kwanza.

 

Hiki hapa kikosi cha kwanza cha Nabi kwenye mechi mbili ambapo hakubadilisha hata mchezaji mmoja katika mchezo wake wa pili dhidi ya Geita Godl baada ya kushinda mbele ya Kagera Sugar:-Djigui Diarra dakika 180, Kibwana Shomari dakika 180, Djuma Shaban dakika 180.

 

Dickson Job dakika 180, Bangala Litombo dakika 180,Khalid Aucho dakika 180,Jesus Moloko dakika 122 bao moja, Yacouba Songne dakika 143 pasi moja ya bao, Feisal Salum dakika 167 bao moja, Fiston Mayele dakika 152.

 

Kwa upande wa wachezaji wake wa akiba ni Heritier Makambo alimpa jumla ya dakika 54, Deus Kaseke dakika 58 na Rajab Athuman dakika 9.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply