The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mastaa wa Kibongo Wafanya Back To School Lamata Village, Wachangia Watoto Wenye Uhitaji

0

Mastaa mbalimbali wa filamu za Kibongo kutoka Lamata Village, jana walishiriki mtoko wa kipekee wa Back To School uliofanyika ndani ya Lamata Village, Goba jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuchangisha fedha na vifaa vya shule kwa ajili ya watoto wenye uhitaji.

Tukio hilo la kijamii lililovutia hisia za wengi liliwakutanisha wasanii, wadau wa sanaa pamoja na wanajamii, ambapo mastaa wote walionekana wakipiga vivazi vya kishule-shule, hali iliyoongeza mvuto na kumbukumbu ya maisha ya uanafunzi.

Akizungumza kwa niaba ya waandaaji, mmoja wa mastaa hao alisema lengo kuu la mtoko huo ni kurudisha tabasamu kwa watoto wanaokosa mahitaji ya msingi ya shule, hususan sare, madaftari, kalamu na ada, huku akisisitiza umuhimu wa elimu kama msingi wa maendeleo ya jamii.

“Tumekutana hapa si kwa burudani tu, bali kwa dhamira ya kugusa maisha ya watoto wenye uhitaji. Kila mchango, mkubwa au mdogo, una maana kubwa kwao,” alisema mmoja wa washiriki.

Katika tukio hilo, mastaa walishiriki michezo midogo, burudani na mawasiliano ya karibu na watoto, huku wakihamasisha wadau wengine kuunga mkono juhudi za kusaidia elimu kwa watoto wasiokuwa na uwezo.

Mtoko wa Back To School Lamata Village umetajwa kuwa mfano mzuri wa wasanii kutumia umaarufu wao kuleta mabadiliko chanya katika jamii, na waandaaji wameahidi kuufanya kuwa tukio la kila mwaka.

Leave A Reply