The House of Favourite Newspapers

Mastaa wa kiume wenye mademu ‘visu’ zaidi Afrika

0

Peter-Okoye-Lola-Okoye

Peter Okoye akiwa na mkewe.

KILA mwanaume anatamani kuwa na mpenzi mzuri, lakini linapokuja suala la mapenzi kigezo cha uzuri wa mtu huweza kuwa na tafsiri pana kiasi kwamba wahenga hawakukosea waliposema kipendacho roho hula nyama mbichi huku Wazungu wakiwa na usemi wa: ‘Beauty is in the eyes of the beholder’ wakiwa na maana kwamba uzuri upo ndani ya macho ya mtu atazamaye.

Lakini misemo yote hiyo bado haiwezi kutengua ukweli kwamba kuna baadhi ya watu huwa wazuri kiasi kwamba uzuri wao unajidhihirisha wazi kwa idadi kubwa ya watu wanaowatazama, vivyo hivyo wapenzi wa mastaa wa baadhi ya mastaa wa kiume barani Afrika, wamekuwa wakitajwa kuwa ni wazuri zaidi Afrika, baadhi yao ni:PAUL OKOYE Ni pacha wa Peter Okoye,pamoja wanaunda kundi la muziki la P.Square nchini Nigeria.

ify-umeokeke-wedding2a

Paul Okoye akiwa na mkewe.

Mwanamuziki huyu ametajwa kuwa na mke mzuri aitwaye Anita Isama ambapo safari yao ya mapenzi ilianzia tangu wakiwa chuo kikuu na kufikia kuoana 2014. Ukimuacha Paul, ukoo huo wa Okoye unatajwa kuwa mvuto wa wanawakewazuri ambapo Peter na kaka yao Jude wote wanatajwa kuwa na wake wazuri lakini hawamshindi mke wa Paul.

10676407_685055688238151_947219946860150880_n

Jose Chameleon akiwea na mkewe.

CHAMELEONE Mkali wa miondoko ya Afro Beat kutoka Uganda,Chameleone ameingia katika listi ya mastaa wenye wapenzi wazuri kupitia mke wake ambaye anafahamika kwa jina la Daniella aliyemuoa mwaka 2008, japokuwa ndoa yao inasuasua kutokana na kile kinachotajwa kama usaliti wa mapenzi unaofanywa na Chameleone lakini wawili hao bado wapo pamoja hadi hivi sasa huku wakiunganishwa na mtoto wao anayechipukia kwenye muziki kwa jina la T-Rex.

BEBE COOL Watu wengi huenda wasifahamu kuwa mkali wa Reggae kutoka Uganda, Bebe Cool ana mke mzuri aitwaye Zuena aliyezaa naye watoto wanne. Wawili hawa walioana mwaka 2014 baada ya kuishi bila kufunga ndoa kwa miaka 12, pamoja wamepitia mengi lakini kuwa kwao pamoja hadi hivi leo kunaonesha jinsi gani wanapendana.

zarinahDIAMOND Staa huyu kutoka TZ,ambaye ana ‘CV’ ya kutoka na ‘watoto’wazuri, alianza kama utani baada ya kutoka na mwanamama mrembo kutoka Uganda, Zari ambaye wakati huo uhusiano wao waliuficha kwenye kile walichokiita ‘Project’.

Baadaye project hiyo ikahamia chumbani zaidi na hatimaye wakapata mtoto (Tiffah) na kuishi pamoja.ICE PRINCE Rapa huyu kutoka Nigeria alitambulishwa Tanzania kupitia ngoma aliyoshirikishwa na mwanadada mrembo Bongo, Jokate Mwegelo inayoitwa Leo Leo,anatajwa kuwa na demu mkali anayejulikana kwa jina la Maima ambaye ni raia wa Ghana.

Wizkid-and-girlfriend-Tania-OmotayoTaarifa zinasema kuwa kupitia uhusiano huo chochote kinaweza kutokea ili kuimarisha penzi lao
motomoto.WIZKID Mkali huyu wa kibao cha Ojuelegba naye anaingia kwenye listi ya mastaa wenye wapenzi wazuri kupitia demu wake chotara ambaye ni muigizaji anayefahamika kwa jina la Tania.

Leave A Reply