Mastaa wa Mwendokasi Festival Wapagawisha Dar
Snura na wacheza shoo wake wakilitawala jukwaa.
Msanii Barnaba Boy akitumbuiza kwenye Tamasha la Mwendokasi usiku wa kuamkia leo.
Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu ambaye alikuwa mshereheshaji (MC) akifurahia jambo na raia wa kigeni.
Msanii Snura akiwa kwenye pozi na meneja wake HK.
Msanii chipukizi akikamua.
Nuh Mziwanda na wacheza shoo wake wakikamua wimbo wa Jike Shupa.
Msanii Rucky Baby akiwa kwenye pozi.
Mashabiki wakifuatilia burudani.
R.O.M.A akifanya yake.
Mchomvu akiwa kwenye pozi.
Rucky Baby akitumbuiza.
MASTAA mbalimbali wa muziki wa Bongo Fleva usiku wa kuamkia leo walitoa burudani kali katika Viwanja vya Posta jijini Dar kwenye Tamasha la Mwendokasi.
Tamasha hilo lilianza majira ya mchana mpaka usiku wa manane likiwa na steji ya kuvutia, misosi mbalimbali na ‘mitungi’ vyote hivyo vikipambwa na mastaa kibao wa muziki huo walioporomosha bonge ya burudani kwa mashabiki wao.
Baadhi ya mastaa waliokinukisha ni Isha Mashauzi, Juma Nature, Rich One, Mabaga Fresh, Man Fongo, G. Nako, Lord Eyes, Navy Kenzo, Snura, Nay wa Mitego, Barnaba Boy na Mbeya City.
Tamasha hilo lilikuwa maalumu kwa uzinduzi wa App ya Klobaa ambayo inampa mpenda burudani nafasi ya kujua maeneo ya kula bata kwa siku husika.