The House of Favourite Newspapers

MASTAA WAIFAGILIA TWANGA PEPETA

Mkurugenzi wa Twanga Pepeta akiwa na wanamuziki Papii Kocha (kushoto) na Dully Sykes (kulia), walipotembelea kwenye usiku wa Twanga Pepeta, The Club Legend.

MASTAA mbalimbali Bongo, hivi karibuni wameifagilia Bendi ya The African Starz ‘Twanga Pepeta’ kutokana na juhudi zake za kurudisha msisimko wa Muziki wa Dansi nchini kama ilivyokuwa hapo awali. Akifungua duru juu ya kukunwa na bendi hiyo mkongwe kwenye gemu la Bongo Fleva, Abdully Sykes ‘Dully Sykes’ aliiambia Global TV Online, kwamba bendi nyingi zimepotea lakini Twanga bado inapeta tena inawanamuziki wakali ambao bado ni vivutio kwa mashabiki.

Naye Petit Man, ambaye ni mzazi mwenza na Esma Abdul, dada wa staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz alisema; “Unajua miaka ya hivi karibuni bendi nyingi zilikimbia mjini na kwenda pembeni, huko ilikuwa ni vigumu kwenda kuburudika, lakini kwa Twanga kuja hapa katikati ya mji msisimko wa dansi unarudi tena.”

Mastaa wengine ambao waliibuka na kuisifia Twanga ambayo kwa sasa safu yake ya waimbaji inaongozwa na Kalala Junior, Chalz Baba, Hadji na wengine wengi, ni Steve Nyerere, Wema Sepetu, Bushoke na Papii Kocha.

Hata hivyo bendi hiyo mwishoni mwa mwezi ujao itakuwa na tamasha kubwa la kuazimisha miaka ishirini tangu kuanzisha kwake na litawaenzi wanamuziki wote waliopita kwenye bendi hiyo na tamasha hilo litafanyika kwenye ukumbi wa The Legend Club (zamani Nyumbani Lounge), inapopiga kila siku za Jumapili.

Stori katika Picha

Petit Man akionyesha upendo kwenye usiku wa Twanga Pepeta, jana.
Wanamuziki wa Twanga Pepeta, Chalz Baba (kushoto), Kalala Junior (katikati) na Luiza Mbutu (kulia), wakiburudisha.
Kalala Junior (kushoto), Papii Kocha (katikati) na Hadji wakiimba Wimbo wa Seya.

Stori: Boniphace Ngumije

 

Comments are closed.