The House of Favourite Newspapers

MASTAA WALIOKUMBANA NA MIFADHAIKO YA AKILI

PAMOJA na mafanikio waliyo nayo mastaa wengi, bado huwa wana matatizo na mifadhaiko ya kimawazo au kiakili.  Kwa vile watu hao wanafahamika zaidi, si rahisi kujificha.  Baadhi yao wakiwemo Demi LovatoCatherine Zeta-Jones, na Jon Hamm,  wameeleza changamoto walizokutana nazo hapo nyuma kuhusu hali hiyo.Tokeo la picha la michelle williams from destiny's child

Michelle Williams

Mwimbaji huyo wa zamani wa kundi la Destiny’s Child amesema aliwahi kutafuta ushauri kuhusu mifadhaiko ya akili na anakiri aliweza kusaidiwa na wataalam wa masuala hayo na kurejea katika hali njema.Picha inayohusiana

Janet Jackson

Mwimbaji huyo maarufu anasema aliwahi kukumbwa na mfadhaiko lakini sasa yuko vyema baada ya kupitia katika furaha na misukosuko kibao.

Kanye West

Aliwahi kukumbwa na mfadhaiko wa akili, hata hivyo anasema yote hayo yamepita, yuko sawa na nguvu kubwa.

Mariah Carey

Mwimbaji huyo aligundulika kuwa na mfadhaiko wa akili mwaka 2001 lakini anasema “hivi sasa niko sawa kabisa”.Tokeo la picha la mel gibson

Mel Gibson

Anakiri kukumbana na mfadhaiko wa akili mnamo mwaka 2011 na anasema hayo ndiyo maisha ambayo watu wengi huyapitia.

PIGO CHADEMA: Mbunge Mwingine Ahamia CCM

Comments are closed.