The House of Favourite Newspapers

Mastaa Waliokuwa Gizani 2019!

0

KUACHIA ngoma kali na kukubalika ni jambo moja, lakini kibarua kigumu zaidi ambacho wasanii wanakuwa nacho ni kuhakikisha wanakuwa juu kila mwaka.

 

Kwenye Bongo Fleva kuna baadhi ya wasanii ambao miaka kama miwili au mmoja uliopita walifanya vizuri, lakini kwa mwaka huu upepo umekuwa mgumu, wameshindwa kuonesha makali yao.

 

Mikito Nusunusu inakuletea orodha ya baadhi ya mastaa ambao mwaka huu, mambo yalikuwa si mambo. Hawakuwika kivile;

 

BARAKAH THE PRINCE

Mwaka huu umekuwa siyo mzuri kwake kutokana na kazi zake kimuziki kuwa tofauti na za kipindi cha nyuma kwani hazikuweza kufika mbali sana kama watu walivyozoea aina ya muziki anaoimba Baraka kufika mbali.

 

Kwa mwaka huu tangu umeanza Barakah hajatoa ngoma yoyote jambo ambalo limefanya mashabiki wake kushindwa kuelewa nini kinaendelea kwa msanii huyo ambaye wamezoea kumuona msanii wao akiwa na kazi kila mwaka.

RICH MAVOKO

Mwaka mmoja tangu alipoachana na lebo iliyokuwa ikimsimamia kimuziki ambayo ni Wasafi Classic Baby (WCB), Mavoko alitoa kazi kadhaa mwaka huu ambazo hazijapata ukubwa uliozoeleka kama kipindi cha nyuma.

 

JIDE

Mkongwe huyu huwa anafanya vizuri sana kutokana na ngoma zake kupendwa na wengi. Mwaka huu umekuwa mbaya kwake kwani hakuweza kusikika kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Kwa mwaka huu, Jide amefanya ngoma ambayo ameshirikishwa na TID inayokwenda kwa jina la Any More, lakini haikufika juu kiivyo.

BOB JUNIOR

Mkali huyu ambaye anaweza kuimba na kutayarisha muziki, yaani prodyuza, amekuwa kimya kwa mwaka huu kiasi cha watu kuanza kumsahau kama anafanya muziki kutokana na kazi zake kutofika mbali kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma kwenye Nichumu na nyinginezo.

DAYNA NYANGE

Mwanadada mwenye umbo ambalo wanaume wengi wamejikuta wakilisifia, mwaka huu amejikuta akipwaya hasa kwenye upande wa muziki na akionekana kuegemea zaidi upande wa biashara. Dayna anaonekana kusafiri sana ndani na nje ya nchi ambapo Mikito Nusunusu iliwahi kumuuliza kuhusu safari hizo kama kuna cha ziada, akasema ni biashara tu na hakuna kingine.

 

 

MABESTE

Ni mkali sana kwenye upande wa muziki wa Hip Hop Bongo, lakini ndani ya mwaka huu hakuweza
waliokuwa gizani 2019!
kuonekana sana kwani kazi zake hazikuweza kufika mbali kama ilivyokuwa kwa wengine kama akina Moni Central Zone na wengine wengi ambao wapo kwenye upande wa muziki wa Hip Hop.

RECHO

Mwanadada huyu aliyekuzwa kwenye Jumba la Vipaji Tanzania (THT) mwaka huu mambo hayakuwa mazuri kimuziki kutokana na kushindwa kutoa ngoma ambayo imebamba kama ilivyokuwa kwenye wimbo wake ule
Kizunguzungu.

CYRIL KAMIKAZE

Singida Boy kama mwenyewe anavyojiita na yeye hakuweza kung’aa mwaka huu kutokana na kushindwa kuwaridhisha mashabiki na wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva kwa jumla ambao wanapenda muziki.

JAY MOE

Huyu ni mkongwe mwenye heshima kubwa kwenye Bongo Fleva. Ameshafanya ngoma kali huko nyuma kama Mvua na Jua, Famous, Nisaidie Kushea, Pesa ya Madafu na nyingine kibao ambazo zilikuwa zinamweka kwenye ramani hata kama anakuwa ana muda mrefu hajaachia ngoma.

 

Mwaka huu amekuwa kimya, haijulikani anatunga sheria gani, lakini mashabiki wake watakuwa wamemmisi kweli.

 

 

Leave A Reply