The House of Favourite Newspapers

MASTAA WAMPONGEZA SHEMEJI YAO UCHEBE!

MASTAA wa filamu Bongo, Jacob Steven ‘JB’, Steven Mengele ‘Nyerere’ na Single Mtambalike ‘Richie’ wamem­pongeza shemeji yao, mume wa msanii mwenzao Zuwena Moham­med ‘Shilole’, Ashiraf Uchebe kwa kumbadili na kumuweka kwenye maadili ya kidini tofauti na alivy­okuwa zamani.

 

Jambo hilo la kumpongeza Uchebe lilichukua nafasi kwenye msiba wa msanii mwenzao Salome Nonge ‘Mama Abdul’ baada ya Shilole kuonekana kubadilika sana kwani hata mmoja wa wasanii alipommwagia pombe kwa bahati mbaya, alionesha kumaindi kuliko maelezo.

 

“Jamani Uchebe hongera sana maana kazi uliyofanya sio ndogo, nakuambia ni kazi kubwa. Yaani dada yetu Shilole leo hii anaona pombe anaruka hivi? Shemeji yetu hongera, umetukosha,” alisema Nyerere huku wote kwa pamoja wakiinuka kwenda kumpa mkoko Uchebe.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO


Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.