The House of Favourite Newspapers

Mastaa Waoga Mamilioni Yanga

0

KIMEELEWEKA! Unaweza kusema hivyo baada ya juzi Alhamisi kutoka na taarifa kwamba mastaa wa Yanga
wamepanga kufanya
mgomo kushinikiza malipo yao ya bonasi, hatimaye mambo yamewekwa sawa
na sasa ni full kicheko
kwao.

Ishu ipo hivi; Alhamisi ya Oktoba 28, 2021, habari kubwa ilisomeka; “Kisa bonasi…


Mastaa Yanga watangaza
mgomo.”Baada ya habari hiyo kutoka, iliwashtua viongozi wa Yanga, fasta wakatinga
kambini na kuweka mambo
sawa ili tu kuondoa sintofahamu ambayo ingeweza kuwafanya waingie kinyonge katika
mchezo wa jana Jumamosi
dhidi ya Azam FC.

Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Kambi ya Yanga iliyopo Avic Town, Kigamboni, Dar, kimeliambia Spoti Xtra kwamba, baada ya viongozi kuona taarifa ile, iliwafanya kufika fasta kambini hapo na kuweka kikao kizito na mastaa hao wakitaka kujua ni nani aliyefichua siri hiyo.


Mtoa taarifa huyo
aliongeza kwamba, katika kikao hicho, mastaa hao wa Yanga walifanyiwa msako wa kutisha ili abainike aliyevujisha taarifa hizo za ukweli na uhakika, lakini hakuna aliyepatikana.

 

Soma ==> Mastaa Yanga Watangaza Mgomo


“Ile habari ya mgomo
ilileta balaa kubwa kambini, viongozi walikuja wakiwa na hasira kweli wakitaka kumjua nani aliyetoboa siri wakati haikutakiwa kutoka nje.


“Wachezaji wote
walisachiwa simu zao, lakini hakuna kilichopatikana. Mwisho wa siku wakazungumza nao kirafiki na kuweka mambo sawa.


“Baada ya kikao cha
kwanza kufanyika Alhamisi, Ijumaa wakaja tena kuongeza hamasa kuelekea
mchezo dhidi ya Azam
ambapo walitoa ahadi kama kawaida yao na kutoa ile bonasi ya mechi mbili kati
ya tatu walizotakiwa kutoa.


“Bonasi iliyotoka ni
ya mechi dhidi ya Geita Gold na KMC ambazo jumla ni shilingi milioni 40 kwa maana ya kila mechi bonasi ya ushindi ni shilingi milioni 20, ile ya Simba ambayo bonasi yake shilingi milioni 400, wachezaji wameahidiwa watapewa Jumatatu baada ya kumalizana na Azam.


“Baada ya kikao
hicho, tabasabu pana kwa wachezaji likaibuka na wakaahidi kutofanya mgomo, huku wakipania kufanya kweli kwenye kila mechi ili kufikia malengo ya kubeba ubingwa msimu huu,” kilisema chanzo
hicho.

Leave A Reply