MASTAA WAPENDANAO WALIOMWAGANA 2018

TUKIWA tumesalia na siku 19 mkononi tuumalize mwaka huu 2018, yapo mengi yametokea kwenye ulimwengu wa mastaa Bongo.

 

Kuna ambao wameanzisha uhusiano mpya, kuna ambao wamemwagana. Makala haya leo yataangazia wale mastaa ambao mapenzi yao yalikuwa moto lakini ndani ya mwaka huu, wamemwagana na kila mtu amechukua hamsini zake:

 

HAMISA NA DAIMOND

Mwanamitindo huyu aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ambapo uhusiano huo ulikuwa wa siri lakini hatimaye walibahatika kupata mtoto wa kiume ambaye baadaye waliingia kwenye mgogoro kuhusiana na matunzo ya mtoto huyo mpaka kufikishana mahakamani lakini walikubaliana. Diamond aliahidi kumtunza lakini hata hivyo, penzi lao ndio liliota mbawa jumla.

LINAH NA SHABAN

Mwanamuziki huyu aliingia kwenye uhusiano na kijana anayeitwa Shaban, takriban miaka mitatu iliyopita na wakabahatika kupata mtoto wa kike aitwaye Tracy lakini wawili hao mwaka huu walivunja mapenzi yao japokuwa walikuwa wameahidiana kuoana.

GIGY MONEY NA MO J

Mwanamuziki huyu naye alianzisha uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji mwenziye Mo J ambaye walikuwa wote wakitangaza Choice FM na uhusiano huo ulikomaa na kuzaa matunda ambapo walibahatika kupata mtoto mmoja wa kike waliyempa jina la Maira lakini wawili hao kwa sasa wameshaachana na tayari Mo ana mwanamke mwingine.

UWOYA NA DOGO JANJA

Staa huyu wa filamu, Irene Uwoya aliingia kwenye ndoa na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ mwishoni mwa mwaka jana. Ndoa yao iliibua maswali mengi kutokana na Uwoya kudaiwa kumzidi umri Dogo Janja.

 

Hata hivyo wawili hao walidhihirisha kuwa ni wanandoa kwa kuishi pamoja pande za Makongo Juu jijini Dar lakini hata hivyo, ndoa yao haikuweza kufika hata mwaka kwani miezi kadhaa iliyopita walimwagana ambapo kwa sasa kila mtu anaendelea na maisha yake.

 

LULU DIVA NA JOH

Mwanamuziki huyu wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume aliyejulikana kwa jina moja la Joh takriban miaka mitano iliyopita lakini mwaka huu walimwagana ambapo mwanaume huyo alimuachia kila kitu Lulu Diva.

TUNDA NA CASTO

Video Queen wa video mbalimbali za wanamuziki hapa Bongo, Anna Kimario ‘Tunda’ na mtangazaji wa Clouds TV, Casto Dickson walianzisha penzi lao na kusumbua mjini kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

 

Penzi lao lilichagizwa zaidi na jinsi Casto alivyojilipua kwa kuchora tatuu ya mrembo huyo l akini hata hivyo, hakuweza kummudu mrembo huyo anayefahamika zaidi kwa kuponda raha mjini, wakamwagana. Kwa sasa kila mtu ana hamsini zake, hakuna hata mmoja kati yao aliyemuanika mpenzi wake mpya.

SAJENTI NA DULLA MAKABILA

Muigizaji Husna Iddi ‘Sajeti’ aliingia kwenye mapenzi na muimbaji wa muziki wa Singeli, Abdul Makabila ‘Dulla Makabila’ l akini mwaka huu walidaiwa kuachana na kila mmoja akaendelea na maisha yake ya kimapenzi.

ZARI NA DAIMOND

Wawili hawa walidumu kwenye uhusiano kwa muda mrefu kidogo na kufanikiwa kupata watoto wawili. Uhusiano wao ulikuwa ni kivutio kikubwa sehemu mbalimbali lakini mwaka huu ndio waliamua kufunga ukurasa wao kimapenzi. Kwa sasa imebaki historia tu huku wakilea watoto ambapo Zari alieleza chanzo cha kummwaga Diamond ni kitendo cha yeye kuwa na michepuko mingi.

Makala: Imelda Mtema

Loading...

Toa comment