Mastaa wavamia kijiji kusaka ugali

MASTAA mbalimbali nchini hivi karibuni walitoa kali ya mwaka baa­da ya kuvamia kijiji cha Ruvu mkoani Pwani kusaka ugali huku kila mmoja akihangaika kivyake ili tu wapate chakula hicho.

 

Tukio hilo lililoshuhudiwa na Ijumaa Wikienda lilitokea wiki iliyopita wakati mastaa hao wa fani mbalimbali walipokuwa kwenye ziara ya kuangalia mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (standard gauge) ambapo staa wa filamu, Irene Uwoya aliweka usistaduu pembeni na kula ugali na samaki aina ya perege kama mtoto wa uswazi.

 

Katika harakati za kupata ugali, Mchungaji Daud Mashimo ambaye pia ni msanii wa filamu alikuwa ni mmoja wa watu walioshiriki mapishi kwani alikuwa mstari wa mbele kwenye kuchochea moto kwa kuweka kuni jikoni ili ugali uweze kuiva.

Pamoja na mchun­gaji huyo, mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shi­lole’, waliingia jikoni huku akiwaomba wanakijiji wa eneo hilo wakae kando am­bapo walibandika maji ya ugali ambao waliuchangia kuusonga.

 

“Yaani hapa mimi nakata kachumbari na wengine waangalie kama samaki zinatosha ili tule ugali mapema kabla treni haijatu­acha jamani, wewe Uwoya ungeenda kumsaidia Mc­hungaji Mashimo kukoleza moto maana hapa vitu ni ku­shirikiana,” alisikika Shilole akitoa maelekezo.

Mastaa hao ambao walichanganyika jinsia tofauti waliacha mshangao mkubwa kijijini hapo kwa sababu wananchi hawak­uamini kile walichokuwa wakikiona kwani wamezoea kuwaona tu kwenye Vituo vya Televisheni na kuamini kuwa wasanii ni mastaa na kwamba hawawezi ku­jichanganya katika maisha ya kijijinijijini.

“Wanaweza kula ugali na samaki wakavu na kachumbari,” dada mmoja alisikika akisema kuonesha mshangao wake kwa mas­taa hao wa Bongo.

Kutokana na kunogewa na ugali mastaa hao wa filamu, muziki, wacheza mpira waliponea chupuchupu kuachwa na treni.

“Tunamshukuru tu Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda (ambaye aliongo­zana nao katika ziara hiyo) kwa kutukusanya pamoja na mambo ya ustaa tumeweka pembeni kabisa hapa ni ugali tu,” alisema Dude.

 

Alhamisi iliyopita mastaa wa fani mbalimbali walitem­belea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasi unaojengwa kutoka Dar mpaka Mo­rogoro kwa awamu ya kwanza ambapo utaendelea hadi Dodoma, Mwanza na Kigoma kwa awamu nyingine.

 

Pia kutumia pesa nyingi unapoanza biashara ni tatizo. Mtu anapotaka kutumia pesa nyingi sana hasa katika kujen­ga taswira badala ya kutumia pesa nyingi katika shughuli za uzalishaji, kuna shida.

Unakuta mtu anaanza biashara tu na anataka kuwa na ofisi kubwa, ananunua samani za bei ghali kwa ajili ya ofisi, komputa za gharama kubwa sana.

 

Kumbuka unapoanza biashara yako, matumizi makubwa ya pesa yako ya­natakiwa yaende zaidi katika vitu ambavyo vina uhusiano wa moja kwa moja na uzal­ishaji wa bidhaa au huduma. Ingawa mwonekano wa nje ni muhimu sana, hautakuwa na maana kama unajenga mwonekano mzuri ila kwenye uhalisia wa biashara hufanyi vizuri.

 

Kila unapotaka kutumia pesa wakati biashara yako ndiyo imeanza, ni lazima ujiulize; je, matumizi ya pesa hii yanachangia vipi kuongeza uzalishaji au faida ya biashara ninayoifanya?

Ukiona kama kila unach­okifanya hakina uhusiano wa moja kwa moja na kuongeza uzalishaji au faida kwenye biashara yako, hasa pale biashara inapokuwa imeanza, unatakiwa ujue kuwa uamuzi huyo yanaweza kuwa chanzo cha kuua biashara yako.

Je, unafikiri kuna sababu yoyote kati ya hizi zi­mechangia biashara yako kutofanya vizuri? Unaweza kunitumia ujumbe mfupi kupitia namba zangu kwa ushauri zaidi.

Stori: Imelda Mtema, Ruvu

Toa comment