The House of Favourite Newspapers

Mastaa wenye vidoti na nyota za ‘ku-shine’

0

snura.jpgMakala: Hamida Hassan

Inawezekana unajua lakini kama ulikuwa bado hujui, nikujuze tu kwamba wapo mastaa watatu Bongo ambao wana vidoti usoni na wamekuwa wachakarikaji katika kuyaboresha maisha yao kupitia fani mbalimbali.

Wengi wanamjua mwanadada Jokate Mwegelo ambaye amekitumia ipasavyo kidoti chake na kufikia kuanzisha kampuni yenye jina la Kidoti Fashions. Makala haya yatakupa orodha ya mastaa watatu ambao wamepambana kuhakikisha wanatumia vipaji vyao kujikwamua kimaisha na wana-shine ile mbaya.

Snura Mushi

Wengi watakumbuka binti huyu alianzia kwenye filamu, akatengeneza jina lake kwa muda mrefu kabla ya kuamua kujichanganya pia na masuala ya muziki.

Kuna wakati alikuwa akifanya vyote kwa pamoja lakini baadaye akaamua kujikita zaidi kwenye muziki. Hapo ndipo alipozidi kupaa hasa kutokana na staili ya muziki anayoimba na lile umbile lake la kufungashia alilolitumia vyema kuwashika mashabiki wake.

Sasa hivi ukizungumzia wasanii wa kike wanaobamba mtaani, jina la Snura haliwezi kukosekana. Kwa upande wa mafanikio Snura mwenyewe anasema amefanikiwa kuwa na kituo chake cha madrasa na kufanikiwa kuwasomesha baadhi ya watoto, si mwepesi wa kutaja mafanikio yake binafsi inabaki kuwa siri yake lakini Snura wa miaka ile wakati anaanza kuigiza siyo huyu wa leo.

Baadhi wanasema kidoti chake siyo ‘orijino’ bali cha kuweka.

Vanessa-Mdee-1Vanessa Mdee ‘V-Money’

Ni kati ya wasanii wakubwa wa kike Bongo wanaofanya vizuri kimataifa. Huyu alianzia kwenye utangazaji, baadaye akajichanganya kwenye muziki.

Ni juzikati tu mwanadada huyo alipata zali la kutwaa Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki kwenye tuzo za Afrimma zilizotolewa kule Marekani na kuwapita wasanii wengi waliomtangulia.

Wapo waliomzungumzia V-Money kama msichana mwenye nyota ya kung’ara kwani tangu akiwa kwenye fani ya utangazaji alipata fursa ya kufanya mahojiano na mastaa wakubwa wa kimataifa huku uwezo wake wa kutema ‘yai’ ukimbeba.

Kimafanikio, siyo mtu wa kujiweka wazi sana lakini kwa anayoyafanya kwenye jamii ni wazi atakuwa amepiga hatua.

Jokate Mwegelo

Ni Miss Tanzania namba 2, 2006. Mara baada ya kushika nafasi hiyo, alianza kujihusisha na mambo ya u-modo huku akifanya pia uigizaji. Ameng’ara kwenye uanamitindo, uigizaji na uanamuziki pia.

Hakuishia hapo, aliamua kitumia kidoti chake kuanzisha ampauni ya Kidoti Fashions inayotoa bidhaa mbalimbali kama vile kandambili na nguo.

Jokate ni kati ya mamisi ambao hawajawahi kuchuja tangu mwaka 2006. Amekuwa mchakarikaji ambaye hakuchoka kutumia kila kipaji alichojaaliwa kuyaboresha maisha yake.

Leave A Reply