The House of Favourite Newspapers

Mastaa Yanga Wafanya Kikao Kizito Usiku dhidi ya Real Bamako ya Mali

0
Wachezaji wa Yanga wakiwa mazoezini nchini Mari.

KUELEKEA mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Real Bamako ya Mali utakaopigwa leo Jumapili, mastaa wa kikosi cha Yanga, jana Jumamosi usiku walitarajiwa kufanya kikao kuweka mikakati mizito ya kuibuka na ushindi.

Yanga leo Jumapili wanatarajiwa kushuka Stade du 26 Mars, nchini Mali kuvaana na Real Bamako katika mchezo wa tatu wa Kundi D la Kombe la Shirikisho Afrika, huku wakiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo uliopita dhidi ya TP Mazembe.

Mpaka sasa katika mashindano hayo, Yanga wanakamatia nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi D, baada ya kukusanya pointi tatu wakicheza michezo miwili, wakishinda mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja.

Akizungumza na Spoti Xtra, Nahodha Msaidizi wa Yanga, Dickson Job, alisema: “Maandalizi yetu ya mchezo dhidi ya Real Bamako yanaendelea vizuri, kama wachezaji tuna ari kubwa na kila mmoja anataka kuhakikisha anapigana kufa na kupona kushinda mchezo huu.

“Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu, lakini kama kikosi tunaamini inawezekana kushinda mchezo huu kama ambavyo tulishinda dhidi ya TP Mazembe, leo (jana) Jumamosi usiku tutakuwa na kikao cha pamoja.”

STORI NA JOEL THOMAS, SPOTI XTRA

NIVA ANA WATOTO 7 WANAWAKE 7, AFICHUA MAPENZI YANAVYOMTESA – ”MIMBA NABEBA MIMI”…

Leave A Reply