The House of Favourite Newspapers

Matatizo ya Uzazi Kwa Wanaume “Male Infertility”-2

0
Couple ignoring each other --- Image by © Lou Cypher/Corbis
Couple ignoring each other — Image by © Lou Cypher/Corbis

Leo naendelea kuelezea matatizo ya uzazi kwa wanaume pamoja na vipimo vya kuyatambua. Endelea…

Kuna wakati mwanaume unatoa mbegu nyingi lakini utaambiwa nyingi zimekufa na nzima ni chache sana, au utaambiwa mbegu zina kasoro, yaani hazina mikia au vichwa vimekatika, hazitembei au kasi yake ni ndogo.

Mambo yanayosababisha tatizo hili ni; ‘Varicocele’ yaani mishipa ya damu kulalia korodani husababisha ongezeko la joto katika korodani au chembechembe nyeupe za damu kujipenyeza ndani ya korodani na kuathiri uzalishaji, pili ni umri mkubwa wa mwanaume unaweza kuwa tatizo katika uzalishaji wa mbegu, mfano umri kuanzia miaka sitini na kuendelea, tatu ni kasoro katika kromozomu zinazotoa jinsia ya kiume ‘Y Chromosome micro deletions’, matatizo mengine yanayoathiri mfumo wa uzazi kwa mwanaume ni kasoro katika mpangilio mzima wa kromozomu mwilini.

‘Klinefelter Syndrome’, saratani au kansa ya mfumo wa uzalishaji mbegu ‘Seminoma’, korodani kutokushuka, kuumia korodani, korodani kujaa maji au busha nalo huathiri uzalishaji wa mbegu, maambukizi ya virusi ndani ya korodani ‘Mumps’, kansa ya korodani yote.

Sababu nyingine hazijulikani. Pia mwanaume anaweza kutoa mbegu nyingi nzima na zenye kasi lakini zikawa hazina uwezo wa kupenya yai.
‘Acrosomal defects’. Pia mwanaume anaweza tu kupungukiwa mbegu za kiume kwa kiasi kikubwa pasipokuwa na sababu yoyote kubwa.
Mionzi ya mara kwa mara katika korodani mfano X-ray huathiri uzalishaji wa mbegu za kiume.

Infertility_MaleInfertility_TreatmentPost Testicular Causes
Hii inahusiana na mwanaume kushindwa kutoa mbegu za kiume akiwa hana tatizo lolote katika uzalishaji, mfumo wake wote wa uzalishaji upo vizuri lakini mbegu hazitoki.
Tatizo hili husababishwa na kasoro au hitilafu katika njia za kutolea mbegu ambazo ni kuziba kwa mirija ya kusafirishia mbegu ‘Vas deferens Obstruction’ kutokuwepo kwa mirija hiyo aidha kwa kukatwa wakati wa upasuaji, ajali au kufunga uzazi ‘Vasectomy’ au mtu kuzaliwa akiwa hana.

Matatizo mengine katika kundi hili ni maambukizi ya mara kwa mara katika viungo vya uzazi vya mwanaume ambayo huambatana na maumivu wakati wa kukojoa, maumivu ya uume, maumivu ya korodani, maambukizi ya tezi dume ambayo huambatana na kutoa manii zenye harufu mbaya, damu kwenye manii.

Tatizo jingine ni kufanya tendo la kujamiiana na kutotoa manii yaani unamaliza tendo lakini manii hazitoki ‘Retrograde Ejaculation’ na ‘Ejaculatory Duct Obstruction’.
Kasoro nyingine inayoathiri utokaji wa manii ni tundu la mkojo katika uume kuwa kwa chini ‘Hypospadias’ tatizo hili hugunduliwa tangu utotoni pia ambapo mtoto akikojoa badala ya mkojo kuruka mbele unatokea kwa chini.

causes-of-male-infertilityUCHUNGUZI WA TATIZO
Uchunguzi hufanyika Hospitali za mikoa katika Kliniki za matatizo ya uzazi. Uchunguzi huzingatia historia ya mgonjwa katika mahusiano na magonjwa mbalimbali yaliyompata awali au yaliyo katika familia yake.
Mambo mengi yataulizwa kufuatana na vyanzo mbalimbali vya matatizo ya uzazi kama tulivyokwishaona.
Mhusika atachunguzwa ukamilifu wa viungo vyake vya uzazi mfano urefu wa uume, tundu la mkojo, korodani zilivyo na kama zimekamilika na endapo hazina tatizo lolote, tezi dume pia itachunguzwa.

Vipimo vya damu kuangalia homoni na maambukizi vitafanyika. Vipimo vya Ultrasound vinaweza kutumika kuangalia korodani kwa undani. Vipimo vya mkojo na mbegu za kiume pia vitafanyika.

UPIMAJI WA MBEGU ZA KIUME
Katika upimaji huu mambo ya msingi yanayoangaliwa ni kiwango cha manii anayotoa ‘Volume of the sample’ ambapo kawaida ni mili za ujazo mbili na nusu hadi tatu na nusu. Jumla ya mbegu anazotoa, zisipungue milioni 20, mwendo kasi wa mbegu kwa kwenda mbele.

Kama unatoa mbegu chache sana utaandikiwa ‘Oligospermia’ au ‘Oligozoospermia’, kama huna kabisa manii, manii hazitoki utakuwa na tatizo la ‘Aspermia’ maana wengine wanatoa tu majimaji hakuna manii wala mbegu.
Utakuwa na ‘Hypospermia’ endapo unatoa kiwango kidogo sana cha manii hata kama mbegu zipo au hakuna

Leave A Reply