The House of Favourite Newspapers

Matatizo Ya Uzazi Kwa Wanaume “Male Infertility”

1

Male_Infertility2‘Male Infertility’ kwa Kiswahili ni ugumba kwa mwanaume, ni hali ambayo mwanaume anashindwa kumpa mimba mwanamke, tatizo hili kwa mujibu wa takwimu huwaathiri wanaume kwa asilimia 40 hadi 50 na huwapata takriban asilimia saba ya wanaume.

Ugumba kwa wanaume kwa kiasi kikubwa husababishwa na tatizo katika uzalishaji na utoaji wa mbegu za uzazi.Tunaposema mwanaume ni mgumba ni pale ameishi na mwanamke kwa mwaka mmoja na tendo la kujamiiana linaendelea kikamilifu lakini hatuoni matokeo. Ingawa tatizo la uzazi lipo pande zote mbili kwa mwanamke na mwanaume, lakini mwanaume pia ana asilimia kubwa ya kuwa na tatizo la uzazi kama ambavyo tumekwishaona hapo awali.

Tatizo hili la uzazi linatokea kwa mtu yeyote bila kujali kama alishawahi kumpa mimba mwanamke au kama ni mwanamke pia haijalishi kama alishawahi kupata ujauzito siku za nyuma. Mtu anaweza kuwa na historia nzuri kuwa alishawahi kumpa mimba mwanaume lakini linaweza kutokea tatizo akashindwa kusababisha ujauzito.

CHANZO CHA UGUMBA KWA MWANAUME
Matatizo ya ugumba kwa mwanaume yamegawanyika katika sehemu kuu mbili, kwanza ni tatizo la kushindwa kufanya tendo la ndoa na pili ni tatizo katika uzalishaji wa mbegu za kiume.

TATIZO KATIKA UZALISHAJI WA MBEGU ZA KIUME
Tatizo hili lipo katika korodani ‘Testicles’ ambapo mwanaume anatakiwa awe nazo mbili, moja kulia na nyingine kushoto. Endapo mwanaume ana korodani moja tu basi ni vizuri akapime mbegu zake kuona kama zipo sawa.

Matatizo ya korodani yamegawanyika katika sehemu kuu tatu, kwanza ni matatizo kabla ya korodani ‘Pre-Testicular causes’, pili ni matatizo ndani ya korodani ‘Testicular causes’ na tatu ni matatizo baada ya korodani ‘Post Testicular factors’. Kwa hiyo mwanaume anaweza kuwa na matatizo yote hayo kuanzia upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume hadi matatizo makubwa katika uzalishaji wa mbegu za kiume.wanaume kama hana kabisa korodani zote mbili basi yeye ni tasa hawezi kumpa mimba mwanamke.

Pre-Testicular causes
Tatizo hili husababishwa na upungufu mkubwa wa vichocheo au ‘hormone’ zinazosaidia au kuchangia uzalishaji wa mbegu za kiume. Matatizo katika hatua hii husababishwa na hali kama vile ‘Hypogonadotropic Hypogonadism’ hapa viungo vya uzazi kama uume na korodani husinyaa na kuwa kama vya mtoto.

Watu wanaoathirika na hali hii ni wale wanene sana ‘Obesity’, watu wenye magonjwa kama ‘Coeliac Diseases’ ambayo ni magonjwa ya tumbo ambapo husumbuliwa na maumivu ya tumbo mara kwa mara, upungufu wa nguvu za kiume na kupoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Chanzo kingine cha tatizo katika sehemu hii ni matumizi ya baadhi ya madawa yawe ya hospitali, ya asili au ya kulevya huathiri kwa kiasi kikubwa uzazi na ndiyo maana inashauriwa unapokuwa na tatizo muone daktari kwa uchunguzi zaidi na tiba.

Walevi nao huathirika sana na matatizo ya uzazi kwani ulevi wa kupindukia huathiri utendaji wa tendo la kujamiiana na uzalishaji wa mbegu za kiume. Kuendesha baiskeli mwendo mrefu na kwa muda mrefu pia ni mojawapo ya vyanzo. Matatizo ya vinasaba ‘Genetic Abnormalities’ nayo huchangia.

Uvutaji wa sigara kwa mwanaume unaathiri uzalishaji wa mbegu za uzazi kwa asilimia thelathini, kemikali zilizomo kwenye tumbaku zimethibitishwa kuua mbegu za kiume ndiyo maana pamoja na madhara mengi ya sigara ndiyo maana makampuni yanayotengeneza sigara huweka onyo kwa wavutaji wa sigara kwamba ni hatari kwa maisha yao.

JINSI SIGARA INAVYOATHIRI UZALISHAJI WA MBEGU ZA KIUME
Mmea wa tumbaku hufyonza madini ya metali yaitwayo ‘cadmium’ toka katika udongo, madini haya hupatikana kwa wingi sehemu zote ambazo tumbaku hustawi.
Itaendelea wiki ijayo.

1 Comment
  1. reuben says

    this an important lesson

Leave A Reply