The House of Favourite Newspapers

Uchaguzi BAZECHA: Suzan Lymo Mwenyekiti Mpya, Hellen Kayanza Katibu Mkuu

  Mwenyekiti mpya wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAZECHA), Suzan Lymo.

WAJUMBE wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAZECHA), wamepiga kura na kumchagua Suzan Lymo kuwa Mwenyekiti wa baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo akiwashinda washindani wengine wanne kwenye kinyang’anyiro hicho.

Suzan anakuwa mwenyekiti mteule wa baraza hilo, akijikusanyia kura 96, huku miongoni mwa aliowabwaga akiwa ni mwenyekiti aliyemaliza muda wake Hashim Issa, aliyepata kura 14 akitetea nafasi hiyo.

Pia wamemchagua Hellen Kayanza kuwa Katibu Mkuu wa baraza hilo (BAZECHA) kwa kura 115 akiwabwaga washindani wengine wawili.

Kabla ya matokeo hayo yaliyotangazwa mapema leo Jumanne Januari 14, 2025, Hellen alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa BAZECHA kwa upande wa Tanzania Bara.

CHADEMA SIMIYU WAMLIPUA MBOWE – WAMUUNGA MKONO LISSU – “TUNATAKA NGUVU MPYA – HATUFUNIKIWI”…