The House of Favourite Newspapers

Matokeo ya uchaguzi wa Liberia: George Weah na Joseph Boakai katika kinyang’anyiro kikali

0

Kiongozi wa upinzani nchini Liberia Joseph Boakai anaongoza kwa asilimia 50.58 dhidi ya Rais George Weah aliye na asilimia 49.42 katika matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais.

Asilimia tisini ya kura zimeshahesabiwa na tume ya uchaguzi nchini humo.

Katika duru ya kwanza ya kura, wagombea hao walishindwa kupata zaidi ya asilimia hamisini ya kura.

Katika duru hii ya pili, mshindi atakayepata kura nyingi kumliko mwenzake hata bila ya kufikisha zaidi ya asilimia hamsini, ndiye atatangazwa mshindi.

Rais Weah anatafuta muhula wa pili madarakani kwa ahadi za kuboresha elimu,ajira na kukabiliana na ufisadi huku bwana Boakai akiahidi kuinusuru Liberia kutoka kwa uongozi mbovu na usimamizi mbaya wa raslimali za nchi unaofanywa na Weah.

Leave A Reply