The House of Favourite Newspapers

Matokeo yampa presha Kingwendu

0

KINGWENDU2

Komediani maarufu Bongo, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’.

Imelda mtema
Pole! Komediani maarufu Bongo, Rashid Mwinshehe ‘Kingwendu’ amesema kuwa matokeo ya uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Kisarawe ambapo alikuwa mmoja wa wagombea, yamemfanya kupata ugonjwa wa presha baada ya kuwa ameshindwa.

Akizungumza na gazeti hili, Kingwendu alisema kipindi chote wakati akisubiria matokeo alikuwa akipata simu nyingi kutoka kwa watu wakiulizia kama ameshinda, hali iliyomfanya apate presha.

“Uchaguzi usikieni tu, siyo kitu cha mchezo hata kidogo. Mimi hapa nimepata ugonjwa wa presha. Pamoja na kukosa lakini najipanga upya kipindi kijacho nitagombea tena baada ya kusomea siasa,” alisema Kingwendu aliyekuwa akigombea kwa tiketi ya Chama cha CUF akiungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Leave A Reply