The House of Favourite Newspapers

Matola apandishwa ndege kusaini dili

0

matolaaKocha Msaidizi,  Seleman Matola.

Mohammed Mdose,

Dar es Salaam

ALIYEKUWA Kocha Msaidizi wa Simba ambaye hivi karibuni aliamua kukaa pembeni kuinoa timu hiyo, Seleman Matola, anaondoka leo Jumatatu kwenda Geita kusaini mkataba na klabu ya Ligi Daraja la Kwanza, Geita Gold Sports.

Matola ametumiwa tiketi ya ndege na klabu hiyo ili aende kumalizana nayo na kusaini mkataba wa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

Championi Jumatatu lilipewa taarifa za Geita kumtaka Matola lakini viongozi wa timu hiyo hawakutaka kuzisambasa mapema kutokana na dili hilo kuwa ndiyo kwanza bado ‘bichi’.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo kilisema uongozi wa timu hiyo inayomilikiwa na kampuni ya kuchimba dhahabu ya mkoani humo, umeamua kumpa Matola dili hilo kutokana na uzoefu alionao kwani wanaamini ataisaidia kuipandisha timu hiyo ligi kuu msimu ujao.

Kilisema kuwa tayari wameshafanya mazungumzo ya awali lakini ni ya juujuu na wamemtaka aende Geita ili wakakamilishe kila kitu.

“Baada ya kusikia Matola hana timu ndipo wakaamua kumuweka kwenye rada zao ili aweze kuipandisha ligi kuu, viongozi wapo tayari kumchukua lakini wanamsubiri yeye tu wafanye nae mazungumzo na kama wakielewana watampa mkataba mara moja,” kilisema chanzo chetu.

Alipotafutwa Matola kuthibitisha taarifa hizo, alitaka kutosema chochote lakini baada ya kuambiwa kuwa zimepatikana kwa viongozi wa timu hiyo, alisema: “Ndiyo wananitaka na tumeshafanya mazungumzo kwa njia ya simu, Jumatatu (leo) watanitumia tiketi ya ndege ili niende kuongea nao kwa kina zaidi na kama tutakubaliana nitaingia nao mkataba.”

Leave A Reply