The House of Favourite Newspapers

Matola Ataja Watakaoiua Yanga Jumamosi

KUREJEA kwa wachezaji wanne wa Lipuli waliokuwa majeruhi ni ishara kwamba Yanga wanalala Jumamosi kwa mujibu wa Kocha wa timu hiyo ya Iringa, Selemani Matola. Timu hizo zitavaana Jumamosi katika Uwanja wa Samora mjini Iringa, huku msimu uliopita Yanga ikifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

 

Wachezaji wa Lipuli ambao wamerejea kutoka kwenye majeruhi ni Miraji Athuman, Paul Ngalema (kadi nyekundu), Gift Mawia na Jamal Mnyate.

 

Lipuli kwa sasa ipo nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na alama 41 baada ya kucheza mechi 30 na kusaliwa na mechi nane tu. Akizungumza na Championi Jumatano, Matola alisema amefurahi kuona kikosi chake kipo fiti ingawa itakuwa sio mechi rahisi kwa upande wao.

“Nafurahi kuona kikosi changu kipo kamili kwa sasa na tayari kwa kupambana sababu wachezaji wangu wanne wamerejea kutoka kwenye majeruhi na mwingine alikuwa na kadi.

 

“Ukweli ni kwamba tunaenda kukutana na Yanga siyo timu rahisi hivyo kujipanga muhimu na tunahitaji kupata matokeo ili kuwa katika nafasi nzuri zaidi,” alisema Matola ambaye baada ya mchezo huo atakimbilia mtaani kuwahi mechi kuitazama mechi ya Simba na AS Vita ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Martha Mboma, Dar es Salaam

Comments are closed.