Matola Kusajili Majembe Mapya 13

KOCHA mpya wa timu ya Polisi Tanzania, Seleman Matola kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara amepanga kukitengeneza kikosi chake kwa kuwasajili wachezaji wapya 13 ambao wataenda kuongeza nguvu.

 

Matola ambaye alijiunga na Polisi Tanzania akitokea Lipuli ya Iringa ambayo ilicheza fainali ya Kombe la FA msimu uliomalizika amekuwa kocha bora na mwenye heshima kubwa kwa siku kadhaa zilizopita.

 

Akizungumza na Championi Jumatano Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi la Polisi, Ali Mtuli alisema kuwa katika kikao walichokaa Jumamosi iliyopita kocha amepanga kusajili wachezaji wapya 13 lakini 10 wengine ni kutoka katika kikosi cha mwanzo.

 

“Kocha amepanga kuwasajili wachezaji wasiopungua 10 lakini nafasi tulizopewa ni 13 wachezaji wapya, kwanza tunataka kuunda timu nzima, kambi bado hatujapanga lakini kuanzia Julai Mosi wachezaji wote wanatakiwa kuanza mazoezi.

 

Kuhusu ishu ya msaidizi wake tunaendelea nayo na hiyo ndiyo ishu kubwa kwetu, tumepanga kumtafutia msaidizi wa hapahapa nyumbani,” alisema Mtuli.

Loading...

Toa comment