The House of Favourite Newspapers

Matola: Mpeni Kagere tuzo yake

Nyota wa Simba Meddie Kagere.

WAKATI Ligi Kuu Bara ikielekea ukingoni kocha wa Lipuli FC, Selemani Matola amefunguka kuwa nyota wa Simba Meddie Kagere anastahili kuwa mchezaji bora katika Ligi Kuu Bara kutokana na kuwa na kiwango bora.

 

Hii ni kutokana na mchango wake ambao ameonyesha na anaendelea kuonyesha ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na michuano ile ya kimataifa iliyopita.

 

Kagere alisajiliwa na Simba msimu huu akitokea kwenye kikosi cha Gor Mahia ya nchini Kenya ambako nako alikuwa moto.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Matola alisema kuwa Kagere ana sifa kuwa mchezaji bora ligi msimu huu. “Kagere wa Simba anastahili kuwa mchezaji bora wa ligi kuu sababu ni mchezaji ambaye ameonyesha kiwango bora na cha hali ya juu msimu huu.

 

“ Ubora wake siyo wa kubeza tumeshuhudia uwezo na kiwango alichoonyesha kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hasa katika upande wa upachikaji mabao tumeona hadi wanatoka amefunga mabao sita.

 

“ Amekuwa ni mchezaji wa tofauti hata ukiangalia umri lakini bado amekuwa akipambana kwa bidii licha ya kuwa mgeni kwenye ligi ya Bongo lakini ameendana na kasi,”alisema Matola. Kagere kwenye ligi kuu kwa sasa ndiyo kinara wa maba ambayo ni 16.

STORI NA MARTHA MBOMA

Comments are closed.