The House of Favourite Newspapers

Matonya ajigamba kumbadilisha Gigy Money

matonya-1STAA kitambo kunako Muziki wa Bongo Fleva, Seif Shaban ‘Matonya’ amejitamba kumbadilisha tabia modo mwenye mbwembwe nyingi, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kupitia wimbo wake wa Hakijaeleweka.matonya-4

Matonya akiwa Global TV Online.

Akizungumza na Global TV Online kupitia kipindi cha Exclusive, Matonya ambaye aliwahi kuwika pia na vibao kibao kama Teksi Bubu, Vaileth na Anita alisema kuwa, mashabiki wengi wa Gigy Money wamezoea kumuona katika muonekano wa kuvaa nguo ambazo si za kiheshima.

matonya-5“Nimeamua kumchukua kwa maksudi Gigy katika video hii ya Hakijaeleweka kwanza, wengi wamezoea kumuona akiwa katika mavazi tofauti ya kimitego f’lan hivi lakini kama ukiangalia katika video yangu naweza kusema najivunia kumbadilisha kitu hicho.matonya-3

…Akiwa na mtangazaji wa Global TV, Kelvin Shayo.

“Anaonekana si Gigy yule aliyezoeleka kutokana na kuvaa mavazi ya kiheshima mwanzo mwisho,” alisema Matonya.

matonya-6…Akiwana mwandishi wa Global Publishers, Nyemo Chilongani.

Matonya pia aliongeza maana ya Wimbo wa Hakijaeleweka kuwa ni kitendo cha mtu unayekuwa naye kwenye uhusiano bila kujua thamani yake na akiondoka ndiyo unajutia na kuona alikuwa na thamani.

matonya-7Matonya akiwa na wafanyakazi wa Global Publishers, Mwandishi Andrew Carlos (wa pili kushoto) na Venant Nicolaus (wa kwanza kulia) na mmoja wa mameneja wake, Capacitor (kushoto).

“Kutokengeneza kiitikio ilinichukuwa muda kidogo lakini zipo baadhi ya sehemu ambazo kiukweli hazikuwa gharama sana ila zilitupotezea muda, kwa mfano kuna sehemu ya makaburini ilituchukuwa muda mpaka tumalize taratibu zote za kuchukua kibali kwa ajili ya kutengeneza video humo,” alimaliza Matonya.matonya-2Akiwa katika picha ya pamoja na Mhariri wa Gazeti la Risasi Jumamosi, Erick Evarist.

Matonya amezungumza mengi, kwa mahojiano utayapata kupitia www.globaltvtz.com

Credit: Andrew Carlos

Comments are closed.