The House of Favourite Newspapers

Matonya awaka kisa, utapeli!

0

MatonyaMkali kitambo kunako muziki wa Bongo Fleva, Seif Shaban ‘Matonya’.

Na Mwandishi Wetu

MKALI kitambo kunako muziki wa Bongo Fleva, Seif Shaban ‘Matonya’ hivi karibuni aligeuka ‘mbogo’ baada ya kuhusishwa na utapeli katika shoo iliyoandaliwa na kituo kimoja cha redio (jina linahifadhiwa) mkoani Iringa.

Akizungumzia na Amani, Matonya alisema kuwa amesikitishwa na uamuzi wa redio hiyo kumtangazia kuwa mmoja wapo kati ya watakaoshiriki katika shoo na kuwa wameshamalizana naye kuhusiana na malipo jambo ambalo halina ukweli.

“Nimesikitishwa sana, shoo ilikuwa tukafanye na Barakah Da Prince, Jay Moe, Bwana Misosi, Mzee Yusuf, FM Academia na wengine wengi, wenzangu walishamalizana lakini kwa nini wanitangazie mabaya kuwa nimemepewa pesa na nimekataa kuhudhuria shoo hiyo,” aliwaka Matonya aliyewahi kutamba na Ngoma ya Vaileth.

Amani lilimtafuta mmoja wa waandaaji wa shoo hiyo ambapo alisema:
“Tulikubaliana kila kitu na Matonya akataka kulipwa zaidi baada ya kuona Baraka amelipwa zaidi yake. ”

Leave A Reply