Matukio Katika Picha Mahakama ya Kisutu Kesi ya Meya wa Zamani ‘Boni Yai’ Iliposikilizwa
Dar es Salaam, 1 Oktoba 2024: Hivi ndivyo hali ilivyokuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini leo wakati Meya wa zamani wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob marufu Boni Yai alipopandishwa kizimbani kwaajili ya kutolewa uamuzi wa kiapo cha ziada kilichokuwa kikizuia meya huyo kuwekewa dhamani. Hata hivyo pingamizi hilo lililowekwa na serikali limetupiliwa mbali.
Meya huyo amerudishwa tena rumande mpaka Oktoba 7 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo kwa ajili ya suala dhamani na kesi mbili zinazomkabili za kusambaza maudhui ya uongo mtandaoni. HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL