The House of Favourite Newspapers

Matukio Katika Picha Ziara ya Mhe. Jaji Kiongozi Mahakama-Pwani

0
Jaji Kiongozi  Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (kulia) akisalimiana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani,  Mhe. Joyce Mkhoi (kushoto) alipowasili mjini Kibaha, April 1, 2020 tayari kwa kuanza ziara ya ukaguzi Mkoani Pwani.
Jaji Kiongozi, Mhe. Dkt Feleshi na Maafisa wa Mahakama alioambatana nao wakinawa mikono kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa ‘corona’ kabla ya kuingia ndani ya jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi , Pwani.
… Dkt. Feleshi (wa pili kushoto) akisalimiana na watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Pwani. Mhe. Jaji. Dkt. Feleshi amewataka Mahakimu na Watumishi wa Mahakama kwa ujumla kuongeza kasi ya usikilizaji wa mashauri ikiwa ni moja ya mbinu ya kukabiliana na ugonjwa hatari wa ‘corona’ unaoikabili dunia.
Mhe. Jaji Kiongozi akizungumza na mmoja wa Wazee wa Baraza (Wa kwanza kushoto) wa Mahakama ya Mwanzo Mailimoja.
Akijadiliana jambo  wakati wa ukaguzi Mahakama ya Mwanzo Msoga. Wa pili kushoto ni Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani, Bw. Moses Minga.
Akizungumza na Mahakimu na Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Mwambao.
Akisalimiana na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Bagamoyo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Bagamoyo, Mhe.Munga Sabuni (aliesimama) akiwasilisha taarifa ya Mahakama hiyo kwa Mhe. Jaji Kiongozi.

 

 

(Picha na Rashid Omar, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Pwani)

Leave A Reply