Baadhi ya maduka yaliyopo mitaa ya Tandale sokoni yakiwa yamefungwa kutekeleza agizo la mkuu wa mkoa wa Dar la kuwataka kufunga maduka yote asubuhi ili usafi ufanyike.
Wakazi wa maeneo ya Tandale Sokoni wakifanya usafi.
Wakazi wa Manzese Darajani wakisafisha ngazi za daraja la wapita kwa mguu.
Wafanyakazi wa Benki ya Akiba Commercial Bank wakiungana na wananchi wa Tandale Sokoni kufanya usafi .
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Akiba Commercial Bank (ACB), Israel Chasosa (wa kwanza kushoto) akiweka uchafu kwenye toroli la taka.
Wafanyakazi wa ACB wakiwa kwenye picha baada ya kumaliza usafi.
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Tundaman (katikati) akiwa na wasanii wenzake wakifanya usafi Tandale Sokoni.
Wakazi wa Tandale wakiwashuhudia wasanii waliokuwa kwenye zoezi la usafi.
Maeneo ya Manzese ‘Tip Top’ yakionekana safi baada ya zoezi la usafi.
Hapa ni Sinza Afrika-Sana baada ya mitaro yake kusafishwa.
Wakazi wa Mbezi ya Kimara wakiongozwa na mwenyekiti wao wa mtaa wa ‘Mbezi kwa Yusufu’, Joseph Mbuya (kulia) wakisafisha eneo lao.
Kina mama wakishiriki usafishaji mazingira huko Mbezi-Kimara.
SHUGHULI ya kufanya usafi nchini ilipamba moto pia katika Jiji la Dar es Salaam kufuatia wito wa Rais Dk. John Magufuli wa kuitumia siku ya uhuru wa Tanzania Bara kwa ajili ya wananchi kusafisha mazingira sehemu za makazi na makazini mwao.
Kamera yetu leo ilitembelea maeneo mbalimbali ambako shughuli hiyo ilifanyika, miongoni mwake yakiwa ni Tandale Sokoni, Manzese Darajani, Mbezi ya Kimara.
PICHA / HABARI: DENIS MTIMA/GPL