Maua Ala Sahani Moja na Yemi Alade

HUWENDA mwaka 2022 ukawa ndiyo safari ya msanii Maua Sama kwenda kimataifa kama Watanzania wengi wanavyotamani kuona.

Hii ni baada ya msanii wa Nigeria, Fiokee kuanika listi ya nyimbo zilizo kwenye albam yake inayokwenda kwa jina la MAN yenye nyimbo zaidi 14 ikiwa na wakali kutoka Afrika.

 

Maua ni miongoni mwa wakali wa Bongo Fleva akiwa wimbo namba 11 wenye jina la Forever akiwa na Lirical.

Mastaa wengine ambao Maua anakula nao sahani moja kwenye album hiyo ni Yemi Alade, Simi, Oxlade, Bella Shmurda, Ric Hassan, Guchi, Chike na wakali wengine.

 

Fiokee anajulikana kama Best Afrobeats Guitarist akiwa ameshiriki kwenye nyimbo za wakali wa Nigeria kama Tiwa Savage, Yemi Alade, Patoranking, Reekado Banks, Adekunle Gold, Flavour, Simi, Kiss Daniel na wakali wengine.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR


Toa comment