The House of Favourite Newspapers
gunners X

MAUA: MWAKA 2018 NIMEJIFUNZA MENGI

MREMBO kunako Bongo Flevani, Maua Sama, aliyetamba na anaendelea kutamba na Ngoma ya Iokote, amefunguka kuwa, anamshukuru Mungu kwa kuwa alitimiza malengo yake ya mwaka uliopita 2018, lakini ulimfanya ajifunze mengi.

Akizungumza na Showbiz Xtra, Maua alisema anaukaribisha Mwaka Mpya wa 2019 vizuri, lakini hatausahau 2018.

“Namshukuru sana Mungu nimemaliza mwaka salama japokuwa nimekutana na changamoto kubwa ambayo sikuitarajia kuipata ile ya kuwekwa ndani kutokana na ngoma hiyo ya Iokote.

“Lakini nashukuru soo liliisha salama na nilijifunza ninatakiwa kuheshimu kila kitu, kwa hiyo sitarajii kitokee kitu kama kile tena katika maisha yangu.

“Kwa sasa ninajikita zaidi kwenye kazi ya sanaa kwa kuwa najua nimejaliwa kipaji na nitatoa kazi ambazo wapenzi wa Maua wanahitaji ili niweze kukonga nyoyo zao,” alisema Maua ambaye alijikuta akiwekwa selo kwa kosa la kuchezea fedha.

Comments are closed.