The House of Favourite Newspapers

Maua Sama Ammwagia Sifa Zuchu

0

BAADA ya Zuchu kusajiliwa kwenye lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), msanii wa Bongo Fleva, Maua Sama ameibuka na kummwagia sifa msanii huyo.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Maua alisema Zuchu ni msanii ambaye alikuwa anamfuatilia kwa muda mrefu na aliona uwezo wake kitambo kuwa anajua muziki, hivyo anamuombea siku moja awe na mafanikio makubwa.

 

“Zuchu mimi nilianza kumfuatilia zamani sana, yupo vizuri, anajua kuimba muziki. Namtakia kila la kheri na ninamuombea mafanikio kwenye kila kitu ambacho anakifanya,” alisema Maua ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Nionyeshe.

STORI: KHADIJA BAKARI, RISASI

Leave A Reply