The House of Favourite Newspapers

Maua Sama Asimulia Alivyotaka Kuacha Muziki

0

Mwanamuziki anayefanya poa kwa sasa katika muziki wa Bongo Fleva; Maua Sama, amefunguka kuwa aliwahi kupitia wakati mgumu kiasi cha kutaka kuacha muziki.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Maua amesema kuwa muziki una changamoto sana na kwa upande wake alipitia vitu vingi kiasi Marehemu Ruge Mutahaba, kumshauri arudi akaajiriwe tu.

 

“Muziki una changamoto, aisee nilipitia wakati mgumu na Bosi Ruge akanishauri nirudi kuajiriwa tu, pengine si mpango wa Mungu kuwa mwanamuziki.

 

Niliumia kwa kipindi hicho, ila sikukata tamaa, nikaendelea mbele kwa sababu nilikuwa napenda sana kuimba na ndiyo kitu kilicho ndani ya moyo wangu,’’ alisema Maua

Leave A Reply