The House of Favourite Newspapers

Mauaji ya Khashoggi: Wasaudi 18 Kuzuiwa Kuingia Ujerumani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Heiko Maas, amesema leo kuwa Berlin itawapiga marufuku raia 18 wa Saudi Arabia kuingia eneo huru la mipaka ya Ulaya kwa visa ya Schengen kwa sababu ya madai ya kuhusika kwao na kuuawa kwa mwandishi wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi.

 

Amesema  ameshauriana na Ufaransa na Uingereza kabla ya kutangaza katazo hilo.

“Kuna maswali zaidi kuliko majibu katika kesi hii, kutokana na uhalifu wenyewe na yule aliyekuwa ameupanga,” Maas amesema katika mkutano wa Umoja wa Ulaya huko Brussels.

 

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema amepewa muhtasari kamili juu ya sauti iliyokuwa imerekodiwa ya mauaji ya mpinzani huyo ambaye ni mwandishi wa habari, yaliyotokea katika ubalozi mdogo huko Istanbul mwezi Oktoba, lakini hana nia ya kusikiliza sauti hiyo iliyorekodiwa kwa sababu ya ukatili wa kile kilichotokea kama kinavyosikika.

 

“Ni sauti ya mateso katika kile kilichorekodiwa. Ni rekodi yenye kuhuzunisha,” Trump ameiambia Fox News Jumapili katika mahojiano yaliyofanyika na kurekodiwa Ijumaa

Comments are closed.