MAUMIVU YA KIFUA NA TIBA YAKE

MauMivu ya kifua ni dalili inayotokea watu wengi mara kwa mara na kati ya sababu inayoleta watu wengi hospitali. Kuna sababu nyingi zinazosabisha maumivu ya kifua, nyingi zikiwa ni hali ambao siyo za kutisha. Wakati mwingine ni ngumu kutofautisha kati ya maumivu ya kifua kutokana na tatizo lenye kuhatarisha maisha na lile ambalo alihatarishi maisha, hivyo muhimu kuwahi hospitali. Chanzo Cha maumivu Kifuani Maumivu ya kifua hutokea kwenye viungo vilivyopo ndani ya kifua. Yanaweza kutoka kwenye sehemu zifuatazo; misuli ya kifua, mbavu, mapafu na mrija wa hewa (trachea), moyo, matiti, mshipa wa damu wa aota na mrija wa chakula (eosophagus).

Maumivu ya kifua huja kwa namna tofauti na kukaa kwa muda tofauti ikitegemea na sababu ya maumivu hayo. Yanaweza kuwa maumivu ya kuchoma au kama kutoboa, maumivu ya kukandamiza au kubana, maumivu ya kuunguza na maumivu butu. Sababu za maumivu ya Kifua Maumivu ya kifua husababisha na mambo mengi, mengine yakiwa ya mpito na yasiyohatarisha maisha. Kuna maumivu

mengine huchangiwa na hali ambazo huweza kuhatarisha maisha ya mhusika. Sababu za kuhatarisha maisha za maumivu ya kifua ni: Mshipa wa aota kupasuka (aortic dissection), shambulio la moyo, nimonia ( pneumonia), damu kuganda kwenye mishipa ya mapafu (pulmonary embolism), mrija wa chakula kupasuka (esophageal perforation), maambukizi ya mfuko wa moyo (pericarditis), hewa, damu au maji kujaa kwenye mapafu (pneumothorax/ hemothorax/hydrothorax) na mfuko wa moyo kujaa maji (pericardial effusion).

Sababu nyingine za maumivu ya kifua ni; kupata ugonjwa wa kifua kikuu (TB), mkanda wa jeshi, kuvunjika mbavu, kiungulia, misuli kuumia kutokana na ajali (muscle strain/injury) na maambukizi ya matiti (mastitis). maumivu ya Kifua KutoKana na matatizo ya moyo Shambulio la moyo na

matatizo mengine ya moyo huleta maumivu ya kifua ambayo ni butu na huwa kama ya kubana au kukandamiza kifua. Utapata maumivu hayo hasa eneo la kushoto na kuhisi maumivu yakisambaa kwenda kwenye kwapa, mkono, bega la kushoto au mgongoni. Hutokea kwa dakika tano mpaka nusu saa.

Mara nyingi maumivu huongezekaunapotembea au kufanya kazi na kupungua ukitulia au kupumzika. Hali hii inaweza kuambata na mgonjwa kupata kizunguzungu, moyo kwenda mbio, kukosa hewa na kichefuchefu. vipimo Uchunguzi wa daktari na vipimo mbalimbali hufanyika kugundua chanzo cha maumivu ya kifua.

Vipimo hivi hujumuisha na picha ya X-ray ya kifua, ECG, Echocardiography, CT Scan ya Kifua na vipimo vya damu. matibabu Matibabu ya maumivu ya kifua hutegemea na sababu ya maumivu hayo. Mara nyingi chanzo kinapojulikana na kutibiwa, maumivu haya hupungua na kuacha. Hata hivyo, wakati mwingine unaweza kutumia dawa za maumivu kupunguza ukali wa maumivu hasa pale unapokuwa umeumia kifua baada ya daktari kukuthibitishia tatizo.

Ikitegemea na sababu ya maumivu, inaweza kuhitaji mgonjwa alazwe kwa uangalizi na matibabu zaidi kama vile kupasuliwa ikiwa mbavu zimevunjika na kusababisha uvujaji wa damu ndani kwa ndani. Usikiapo maumivu ya kifua nenda haraka ukaonane na mtaalamu wa afya ambaye atakupima na kugundua tatizo.


Loading...

Toa comment