The House of Favourite Newspapers

MAUMIVU YA KORODANI CHANZO CHA KUTOPATA MTOTO -3

Tunaendelea na mfululizo wa mada yetu inayohusu maumivu ya korodani chanzo cha kutopata mtoto. Endelea…

TATIZO linapotokea katika utu uzima huambatana na upungufu wa nguvu za kiume, kusinyaa korodani na uume kuwa mfupi au mdogo. 

 

Hii ni kutokana na korodani kushindwa kuzalisha vichocheo au homoni za kiume kama tatizo ni tangu balehe, basi hali ya matatizo makubwa hutokea katika mfumo wa uzazi na mwili kwa ujumla. Hayo ni baadhi tu ya matatizo ila mengi tutaendelea kuyaona.

 

Korodani kushindwa kufanya kazi husababishwa na matatizo mengi kama vile matumizi ya madawa baadhi yake ya hospitali kwa muda mrefu hasa kwa wanaume mfano dawa za jamii ya Glucocorticoids, Ketoconazole, na mada wa ya kulevya hasa bangi.

 

DALILI ZA TATIZO

Endapo korodani zako zinashindwa kuzalisha mbegu za kiume utajikuta unaishi na mke kwa zaidi ya mwaka mmoja na mnafanya tendo la ndoa kwa lengo la kutafuta mtoto na mnakosa.

 

Endapo korodani zinashindwa kuzalisha homoni za kiume basi kutakuwa na dalili zifuatazo, kama ni mtoto anakuwa harefuki anaendelea kuwa mfupi huku umri unaenda, matiti ya mtoto wa kiume au kijana yanakuwa makubwa Gynecomastia mwili hauwi na misuli imara, kukosa hamu ya tendo la ndoa, unakuta vinyweleo vya kwapani na sehemu za siri havioti au kama vilishaanza kuota havikui hata kwa zaidi ya mwaka, huoti ndevu na kubadilika kama mwanaume, uume haukui na korodani zinasinyaa na kuwa kama za mtoto. Sauti haiwi nzito.

UCHUNGUZI

Matatizo ya viungo vya uzazi huchunguzwa katika hospitali za wilaya na mkoa, uchunguzi wa awali hufanyika kwenye vituo vya afya.Vipimo mbalimbali hufanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa.

 

USHAURI

Matibabu huchukua muda mrefu baada ya uchunguzi wa kina. Matibabu ya dharura hufanyika pale kunapokuwa na maumivu makali. Ni vema kuepuka maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa na kuwahi hospitali pale unapohisi una tatizo.

Comments are closed.