The House of Favourite Newspapers

Maumivu ya tumbo ya mara kwa mara kwa wanawake

0

Acute-AbdomenInaendelea kutoka wiki iliyopita

Maambukizi nje ya kizazi humfanya mwanamke aumwe tumbo lote na kupata hali iitwayo ‘Perionitis’, hupata homa za mara kwa mara na mwili kuwa mnyonge.Maumivu ya muda mrefu hudhoofisha afya ya mwanamke, hukosa hamu ya kula na kupoteza raha ya tendo la ndoa na uzazi husumbua.

Maambukizi hushambulia kwa njia ya kupitia ukeni, mfano magonjwa ya ngono, kuharibika au kutoa mimba na hata kwa kufanyiwa upasuaji wa tumbo pia huathiri mfumo wa uzazi.Vyanzo vingine vinavyoathiri mfumo wa uzazi na kusababisha maumivu ya chini ya tumbo mara kwa mara ni matatizo katika mfumo wa homoni au vichocheo, uvimbe katika kizazi, mirija na vifuko vya mayai.

ATHARI ZA TATIZO
Maambukizi sugu katika mfumo wa uzazi huathiri mzunguko wa hedhi, uzalishaji mayai ya uzazi, kuziba mirija ya uzazi, kupoteza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa.
Kwa ujumla mwanamke mwenye tatizo hili anaweza kupoteza uwezo wa kuzaa na kuwa mgumba.
Matatizo haya hutokea zaidi kwa mwanamke aliye katika umri wa kuzaa.

UCHUNGUZI
Matatizo haya hufanyiwa uchunguzi katika kliniki za magonjwa ya akina mama. Vipimo mbalimbali vitafanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa.
Matibabu/Tiba inaweza kuwa dawa, upasuaji au yoyote ambayo daktari ataona inafaa kutegemea aina na ukubwa wa tatizo.

Leave A Reply