Kartra

Mauzauza Yatishia Usalama Hospitali ya Nkasi

UONGOZI wa Hospitali ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa umelalamikia vitendo vya ushirikina vinavyofanywa hospitalini hapo kiasi cha kuhatarisha usalama kwa wafanyakazi wa hospitali hiyo.

 

Akitoa taarifa kwenye kikao kazi kilichojumuisha wataalamu,viongozi wa ngazi ya jamii na wakunga wa jadi leo ambapo mganga mkuu wa hospitali hiyo Martha Chacha alidai kuwa hari iliyopo sasa inatisha ambapo watendaji wa hospitali hiyo wamekuwa wakitishwa na mauza mauza yaliyopo katika hospitali hiyo hasa nyakati za usiku.

Alisema kuwa vitendo hivyo vya kishirikina vimekuwa vikififisha hari ya kufanya kazi kwa wafanyakazi wa hospitali hiyo kwa maana wauguzi, manesi na wengineo wawapo zamu za usiku ukwamishwa kufanya kazi zao kwa kukumbana na mauza uza kama.

 

Ameyataja mauzauza hayo kuwa ni kama vile kuvutwa miguu na kitu kisichoonekana, kuzima taa na kuziwasha wakiwa wanatoa huduma mbalimbali kwa wagonjwa.

 

Mganga huyo alisema kuwa hivi watumishi wengi wa hospitali hiyo ukataa kupangwa zamu za usiku na kuifanya kazi yao.


Toa comment