Mawakala wa Bima Wafanya Mkutano Kujadili Changamoto, Kamishna Awaahidi Neema
Dar es Salaam 7 Desemba 2022: Viongozi wa mawakala wa bima nchini kutoka kanda tano za Tanzania Bara pamoja na Zanzibar leo wamefanya mkutano mkuu kujadili changamoto ya kazi zao.
Mawakala hao pamoja na kujadili changamoto hizo waliziwakilishwa kwa Kamishna Mkuu wa Bima nchini, Baghayo Saqware aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mkutano.
Akizungumza na viongozi hao wa mawakala kamishna Saqware alianza na kuwapongeza mawakala hao kwa kuendelea kutoa huduma za kiuminifu kwa wateja wao na kuwaambia kuwa changamoto zao zote amezipokea na kuwaahidi kuzifikisha kwenye mamlaka husika ikiwemo kwa waziri kwa ajili ya kuzifanyia utatuzi.
Viongozi hao wa mawakala hao kwa kuonesha kujali umuhimu wa bima nao wamezindua mfuko wao wa bima itakayotolewa na Bumaco kwa ajili ya familia zao na watumishi wao.
Kamishna huyo aliwataka viongozi hao kuboresha mazingira ya ofisi kwani neema zaidi inakuja ikiwemo kuanza kutoa huduma ya bima ya afya ambayo inatarajiwa kuwa kwa kila mwananchi. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY /GPL