Mawaziri Wa Magufuli Wafungiwa Kazi, Ripoti Kamili Ipo Hapa

 lukuvi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Na Waandishi Wetu, Ijumaa, Januari 6-12, Toleo na 1019

DAR ES SALAAM: Ikiwa imetimia mwaka mmoja na ushee tangu Rais Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ awe madarakani baada ya kuapishwa Novemba 5, mwaka juzi, mambo mbalimbali yamezungumzwa kuhusu utendaji wake unaosifika kwa kiwango kikubwa na wananchi wa kada mbalimbali nchini.
Licha ya sifa binafsi kwa Rais Magufuli mwenyewe kama Mtendaji Mkuu, pia baadhi ya mawaziri wake nao wametajwa kama miongoni mwa watu wanaofanya kazi kwa spidi yake, wakiongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa, jimbo linalopatikana mkoani Lindi.

ijumaa-1
Ukiondoa Waziri Mkuu Majaliwa, mawaziri wengine ambao wadau wanaamini wanafanya kazi kubwa wakifuata nyayo za Magufuli, ni pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na yule wa Biashara na Viwanda, Charles Mwijage.

majaliwa-3

Waziri Mkuu Majaliwa.

Wengine wanaotajwa kwenda sambamba na kasi ya Rais Magufuli ni pamoja na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Naibu wake, Dk. Hamis Kigwangalah, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Anjela Kairuki pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) George Simbachawene na Naibu wake, Suleimani Jafo.

simbachawene-stori-1

Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) George Simbachawene.

Hata hivyo, licha ya mawaziri karibu wote kufanya vizuri pia, kumekuwepo na manenomaneno kutoka kwa watumishi wa chini juu ya uchelewaji wa kuingia kazini kwa baadhi ya mawaziri, uchelewaji wa kuchukua hatua na wengine, wakidaiwa kutumia muda mwingi ofisini badala ya kuwa kwenye maeneo ya matukio kutegemea na majukumu yao.

mpango

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango.

NINI MAANA YA KUCHELEWA?
Kuchelewa ni kitendo cha mtu kupitisha muda wa kuingia kazini bila kujali kama alitoa udhuru au la! Hata kama mtu akiwa amepitia kumwona mgonjwa mahali halafu akachelewa kuingia ofisini, ni kuchelewa tu. ndiyo maana utamsikia mtu akisema: “Leo nilichelewa kuingia kazini, nilipitia hospitali.”

MUDA WA KUINGIA KAZINI SERIKALINI
Kwa serikali, muda rasmi wa kuingia kazini ni saa1:30 asubuhi na ndiyo hata daftari huanzwa kusainiwa mpaka wakati huo kabla ya kupigwa mstari kuashiria kwamba, watakaofika zaidi ya hapo watakuwa wamechelewa.
waziri-3

Gari la Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

OFM YAINGIA KAZINI
Lakini ili kujiridhisha na manenomaneno hayo ya uchelewaji wa kuingia kazini, kitengo maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers, kiliamua kuwafungia kazi viongozi hao wa juu kwa siku mbili mfululizo, ili kubaini muda wao wa kuingia kazini kama kuna wanaochelewa bila kujali udhuru au la!
muhongo

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

OFM WAJIPANGA, ALFAJIRI DESEMBA 21, 2016
Makamanda wa OFM waliamka alfajiri na ilipofika saa kumi na moja kamili, walikuwa nje ya wizara nne kwani licha ya madai ya kuchelewa kuingia kazini, wapo pia baadhi ya mawaziri waliowahi kufika kazini ili kutimiza majukumu yao kwa wakati.
WIZARANI KWA PROFESA MUHONGO
Kamanda aliyekuwa ndani ya eneo la wizara hiyo, iliyopo Mtaa wa Samora katikati ya Jiji la Dar es Salaam, alianza kuwaona wafanyakazi wakianza kuwasili kuanzia saa 12 asubuhi, wengi wao wakija na magari ya serikali yaliyokuwa na namba za usajili STK na kufikia saa mbili na nusu, gari za kuingia kwenye jengo hilo la ghorofa nane zilitimia.

1.Wazri wa afya,Jinsia wazee na watoto,Ummy Mwalimu akisoma hotuba yake.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu (kushoto).

Kwa kuwa magari ya mawaziri na manaibu wao huwa na namba maalum zinazotambulisha vyeo na wizara, hadi wakati huo, hakukuwa na gari la Waziri au Naibu wake lililokuwa limefika ofisini. Hata hivyo, baadaye ilibainika kuwa, Naibu Waziri Dk. Medard Kalemani alikuwa safarini.
Ilipofika saa 3: 33 gari lenye namba za Waziri wa Nishati na Madini (W NM), likiwa na vioo vya giza, liliingia katika lango kuu na kutokomea ndani, bila kamanda wa OFM kubaini kama aliyekuwepo garini ni Waziri Sospeter Muhongo au la.
waziri-1

MPINGO HOUSE ‘WAZEE WA FARU JOHN’
Katika Wizara ya Maliasili na Utalii, iliyo na ofisi zake katika Barabara ya Nyerere, eneo za Bohari Kuu ya Madawa ambayo imekuwa maarufu siku za hivi karibuni kutokana na sakata la Faru John, makachero wa OFM, walimshuhudia Waziri Profesa Jumanne Maghembe akiwasili ofisini kwake majira ya saa 2:30 akiwa kwenye gari lenye namba W MU (Waziri Maliasili na Utalii).
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mahmoud Mgimwa, naye ilithibitika kuwa alikuwa safarini.

waziri-4

Gari la Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe.

WIZARA YA MAMBO YA NDANI
Ofisi za Wizara hii ambayo ipo katika makutano ya barabara ya Ohio na Gerezani, makamanda wetu hawakuweza kuwaona Waziri wala Naibu wake kwa maelezo kuwa, walikuwa kwenye kikao Ikulu ya Rais John Magufuli, lakini waliweza kumbaini bosi wa mapolisi, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu akiwasili mishale ya saa 1:52.

OFM KAZINI DESEMBA 22, 2016
Ili kuendeleza uchunguzi wake katika wizara mbalimbali, kesho yake, Desemba 22, mwaka jana, OFM waliingia tena kazini mapema alfajiri na safari hii, wakajiegemeza katika wizara mbili ili kubaini muda ambao mawaziri wake wanaingia kwenda kuwajibika kwa umma.

721

Naibu Waziri wa Fedha, Dk. Ashatu Kijaji (NW FM).

KILIMO, MIFUGO, UVUVI NA UMWAGILIAJI
Katika ofisi za wizara hii zilizopo eneo la Tazara Vertinary, nje ya jiji ambayo bosi wake ni Dt. Charles John Tizeba, kamanda wa OFM alielezwa kuwa mbunge huyo wa Buchosa mkoani Mwanza, alikuwa safarini kikazi, lakini Naibu wake, William Ole Nasha alionwa na OFM akiingia ofisini majira ya saa 2: 01 (NW MUU).

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
Katika wizara hii ambayo ndiyo imebeba roho ya Watanzania, iliyo na ofisi zake katika Mtaa wa Mirambo katikati ya Jiji la Dar es Salaam, bosi wake, Waziri Dk. Philip Mpango alifika kazini hapo majira ya saa 1:40 na gari lenye namba W FM (Waziri wa Fedha na Mipango) ikiwa ni dakika saba baada ya kuwasili kwa Naibu wake, Dk. Ashatu Kijaji (NW FM).
OFM inaendelea kufanyia kazi muda ambao mawaziri na viongozi wengine wa juu wanawasili katika maeneo yao ya kazi, sambamba na malalamiko mengine yanayoletwa ili kuhakikisha watumishi hao wanafanya kazi kwa mujibu wa taratibu kama anavyotaka Magufuli.

halotel-strip-1-1

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment