The House of Favourite Newspapers

Maxime aanza hesabu za ligi kuu

0

mecky-Maxime Mecky Maxime.

 

Martha Mboma,

Dar es Salaam

KIKOSI cha Mtibwa Sugar kimeanza mazoezi yake rasmi juzi Jumatatu ufukweni kuhakikisha kinajimarisha vyema na kuweza kupambana na mikikimikiki ya Ligi Kuu Bara huku kikiweka kando suala ya usajili kwa muda.

Mtibwa inayonolewa na Mecky Maxime, kwa sasa inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na alama 22 nyuma ya Yanga yenye alama 23.

Akizungumza na Championi Jumatano, ofisa habari wa timu hiyo, Thobias Kifaru, alisema kikosi hicho kitajifua kwa wiki mbili jijini Dar kisha kurejea Manungu kwa maandalizi zaidi.

“Timu inafanya mazoezi Dar kwa wiki mbili, imeanza juzi kwa mazoezi ya ufukweni lengo ni kuhakikisha tunafanya vyema kwenye ligi na kuweza kushika usukani, masuala ya usajili tutatoa taarifa, kwa sasa tumeyaweka kando kidogo lakini kama kutakuwa na lolote tutasema,” alisema Kifaru.

Leave A Reply