The House of Favourite Newspapers

Maya Atoa Sababu Ya Kutomposti Lulu

0
Mayasa Mrisho ‘Maya’ (kulia) akiwa na msanii mwenzake wa Bongo movies Shamsa Ford

MUIGIZAJI mkongwe wa Bongo Muvi, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefungukia sababu za kutoposti picha yoyote ya msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ kipindi akiwa anasubiria hukumu yake kama walivyofanya mastaa wengine.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi Maya alisema kuwa yeye kutofanya hivyo ni kwa sababu hata akimposti mtu haimaanishi kuwa ndiyo inatoka moyoni anaweza akawa anadanganya maana ukweli uko ndani ya moyo.

 

 

“Siyo lazima mimi kumposti Lulu kwa kufuata watu tu wanavyofanya, kila mtu ana ukweli wake ndani ya moyo maana hao waliomposti kumpa pole wanaweza kuwa ni waongo lakini mimi naweza kuwa sijafanya hivyo na nikamaanisha ndani ya moyo wangu” alisema Maya.

Na Imelda Mtema

Leave A Reply