MAYA: WANICHEKE TU, MI SIKURUPUKII MTOTO

Mayasa Mrisho ‘Maya’

MSANII wa kitambo kwenye ulimwengu wa filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amesema kuwa hata kama wenzake watamcheka kwa sababu mpaka sasa hajapata mtoto, hatokurupuka kumsaka kwa sababu ya matakwa ya watu.  Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Maya alisema kuwa anajua wasanii wenzake wengi wana watoto na wapo wanaomcheka na kumshangaa lakini sababu hiyo pekee haiwezi kumfanya yeye akakurupuka kumsaka kwa udi na uvumba.

“Yaani siwezi kuharakisha kwenye suala la uzazi kabisa, hata nikizaa na miaka hamsini haina shida ili mradi tu nizae na baba mwenye kupenda mtoto na kutoa matunzo bora kwa ajili ya mwanangu,” alisema Maya.

Stori: Imelda Mtema


Loading...

Toa comment