The House of Favourite Newspapers

Mayanja azitunishia misuli Yanga, Azam

0

Khadija Mngwai, Dar es Salaam
KOCHA Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja, amefunguka kuwa ligi ya msimu huu bado ipo wazi na yeyote kati ya timu nne za juu ana nafasi ya ubingwa huku akitamba kwamba atazidi kwenda bega kwa bega na wapinzani wao Yanga na Azam hadi kieleweke.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Mayanja amesema Simba bado ina nafasi ya kutwaa ubingwa wa ligi kufuatia hali halisi ya ushindani iliyopo ambapo kuanzia timu iliyoshika namba moja hadi nne zote zina nafasi ya kutwaa ubingwa kwa kuwa hazijaachana sana.

“Siwezi kulizungumzia suala hilo kwani hadi sasa haijajulikana nani anaweza kuchukua ubingwa kwani kuanzia timu iliyo namba moja hadi nne zina nafasi ya kutwaa ubingwa kutokana na ushindani uliopo hivi sasa.

“Hivyo sina wasi na hilo kwani timu yangu naamini itafanya vyema, lolote linaweza kutokea na ninakiandaa kikosi changu kiweze kufanya vizuri katika mechi zilizo mbele yetu kuhakikisha tunaibuka na ushindi,” alisema Mayanja ambaye tangu achukue mikoba ya Muingereza, Dylan Kerr ameshinda mechi saba za ligi (kabla ya jana) na kufungwa mchezo mmoja dhidi ya Yanga, huku akishinda michezo miwili ya FA.

Leave A Reply