Mayele Atangaza Hali ya Hatari, Awapania Dodoma Jiji

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele

MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, ameweka wazi kuwa licha ya kupoteza mkwaju wa penati katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons Jumatatu iliyopita, straika wao, Fiston Mayele hana presha yoyote na amejipanga kuwanyamazisha wakosoaji wake kwa kufunga mabao mengi zaidi kwenye michezo ijayo.

 

Jumatatu wiki hii Yanga wakiwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam walilazimishwa suluhu dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, huku tukio la Mayele kukosa penalti likizua mjadala mkubwa.

 

Suluhu hiyo ilikuwa ni ya tatu mfululizo kwa Yanga ambayo imewafanya wafikishe pointi 57 na kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, baada ya kucheza michezo 23.

Fiston Kalala Mayele akipiga mpira wa kichwa kwenye pambano dhidi ya Ruvushooting

Akizungumza na Championi Ijumaa, Mwakalebela alisema: “Kwanza kabisa niwatoe hofu mashabiki wetu kuwa hali ni shwari na hakuna changamoto yoyote kwenye kikosi kwa sasa, ni kweli hatujawa na matokeo mazuri katika michezo yetu mitatu iliyopita lakini tunaendelea kupambana kufanikisha malengo yetu.

 

“Ishu ya kukosa penalti inaweza kutokea kwa mchezaji yeyote na wala hakuna presha yoyote iliyowekwa kwa Mayele kwa sasa, zaidi sana amejipanga vizuri kuendeleza moto wake wa kufunga mabao na kuwanyamazisha wale wote ambao wanamkosoa kwa sasa.”

 

Joel Thomas

 

 

 

 

 

 

 706
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment